📌RHODA SIMBA
WAZIRI wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Selemani Jafo ameteua Wajumbe14 washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi shindani Duniani katika kutunza Mazingira.
Aidha katika orodha ya mabalozi hao imejumuisha waandishi wa habari Sakina Abdulmasoud,Aboubakari Famau,pamoja na Oliver Nyeriga ambao ni wanachama wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ( CPC) .
Sakina Abdul Masoud mwandishi kutoka Uhuru Media Groupambaye pia ni mwanchama wa Central Press Club ni miongoni mwa mabalozi 40 walioteuliwa na Waziri Jafo. |
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Waziri huyo amesema kampeni hiyo imekuja baada ya maeneo kama vile maziwa na bahari kiwango cha maji kimepanda kutokana na uchafuzi wa mazingira katika maeneo hayo.
Kampeni hii ya Mazingira kwa Mwaka huu itahusisha kila Idara,zikiwemo Taasisi,Mikoa pamoja na Wilaya,kata vijiji na Mitaaa,Viwanda migodi na maeneo mbalimbali wakiwemo wadau wa Usafi na itaungana na utoaji wa tuzo mbalimbali kwa Washindi wa uandishi wa Habari za Mazingira
Waziri Jafo.
Amesema kampeni hiyo
ya Mazingira yenye kaulimbiu isemayo Mazingira yangu,Tanzania Yangu,Nakupenda Daima itazinduliwa rasmin June 5 mwaka huu siku ya Kilele Cha
maadhhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambapo mgeni rasmi atakuwa
Makamu wa Rais DK.Philip Mpango Mkoani Dodoma huku akisema kampeni hiyo
itakuwa endelevu.
Nana tarajia kukutana na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika na mazingira mnamo mei 27 Jijini Dodoma kwa lengo la kuiwezesha kampeni hiyo.
Hata hivyo
Mabalozi 40 aliowateua wakiwemo wasanii pamoja na Waandishi wa Habari akiwemo
Msanii Diamond platnums na Harmonize.
0 Comments