📌RHODA SIMBA.
WAHANDISI wametakiwa kukamilisha miradi yote mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na serikali ya awamu tano kwa lengo la kukuza uchumi na kujenga Tanzania ya viwanda.
Aidha katika mwaka wa fedha 2021/2022 serikali imetenga Sh. Tilioni 4 kwaajili ya miradi ya ujenzi ambayo imepangwa kutekeleza hapa nchini.
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Joseph Malongo wakati akifungua warsha ya siku tatu kwa wahandisi nakuitaja miradi hiyo kuwa ni Daraja la Salenda,Daraja la Busisi, Miradi wa kufua umeme na Reli ya kisasa
"Serikali iliyopitia iliandaa miradi mikubwa ya kimkakati na serikali ya awamu ya sita imeahidi kutekeleza, waandisi mnajukumu kubwa la kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kwasababu kukamilika kwake itakuwa ni chachu ya maendeleo kwa Taifa,
"Kwa nchi hizi ambazo bado zinaendelea sekta ya ujenzi ni muhimu sana kwasababu inachangia asilimia kubwa ya maendeleo ya viwanda na biashara hivyo kuongeza ukuaji wa uchumi," amesema
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wahandisi Prof Ninatubu Lema amesema wamejipanga kuhakikisha wanashirikiana na serikali kukamilisha miradi yote mikubwa ambayo tayari ilishaanzishwa.
Amesema serikali imewapa jukumu hilo la utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo hivyo nao watajitahidi kuhakikisha wanakwenda kufanya kazi hizo kwa weledi mkubwa hasa ukizingatia taifa linakwenda kasi ili kukuza uchumi wa nchi.
Tunaishukuru sana serikali kwa kutuamini wahandisi,ndio maana tumeandaa warsha hii ili kujadili mambo mazuri ya uendeshaji miradi nasi tutaishauri serikali nini kifanyike ili tukamilishe miradi kwa wakati
"Pia sisi wahandisi zaidi ya 30,000 tunaahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hasan na kushirikiana nae katika shughuli mbalimbali za ujenzi na kutekeleza miradi ambayo itakuwa na manufaa kwa taifa,
Prof Lema amewataka wahandisi kujiongeza kielimu wao wenyewe ili waweze kuendana na wahandisi waliko katika sehemu nyingine ambazo wanauwezo wa kufanya kila aina ya kazi na kuwahasa kutobweteke katika kazi ya aina moja
Naye Msajili wa Wahandisi Mhandisi Patrick Barozi amesema mafunzo hayo yataenda sambamba na kutafakali chanzo cha wahandisi wengi wa miradi ya maji kushindwa kutekeleza miradi hiyo kwa wakati na kufanya wahandisi wote nchini kuongelewa vibaya na jamii.
Amesema ukiachana na miradi mikubwa ambayo inatekelezwa hapa nchi ipo miradi ya maji ambayo ilitekelezwa na wahandisi lakini hadi Leo haifanyi kazi katika warsha hii watajua tatizo lilikuwa wapii
" Kwa upande wa
miradi ya maji malalamiko yamekuwa mengi hasa yakienda kwa wahandisi, sasa
kwenye warsha hii tutajua kwanini malalamiko yanakuwa mengi na tatizo liko wapi
na nini kifanyike ilikuondoa malalamiko hayo,"ameeleza
0 Comments