📌RHODA SIMBA
WADAU wa elimu wameiomba Serikali kuweka uwiano wa walimu shuleni kwa kuzingatia makundi ya watoto wenye ulemavu lengo likiwa ni upatikanaji wa fursa ya elimu bora kwa watoto wenye uhitaji maalumu ya kielimu.
Hayo yamesemwa leo jijini hapa na Afisa Jeshi la Polisi dawati la jinsia na watoto Teresia Mdendemi wakati akichangia mada katika warsha ya wadau wa elimu jumuishi ambapo,Mada hiyo iliyowasilishwa na mshauri mwelekezi kutoka Haki elimu Wilberforce Meena.
Tunaona watoto wenye uhitaji maalumu wana uhitaji maalumu kutokana na hali waliyo nayo tunaamini serikali yetu ni sikivu sana kwahiyo tunaomba kila mtoto apate haki yake ya kielimu
Aidha kwa upande wake Meena amesema sera ndio inayoongoza mfumo mzima wa elimu hivyo sera iliyopita haijaweka bayana kuhusu elimu jumuishi inayolenga makundi maalumu hivyo wao kama haki elimu wametoa mapendekezo kwa serikali mara baada ya kutangaza mchakato wa kupitia sera ya elimu.
"kama shuleni mtoto mwenye mahitaji maalumu hafundishwi vizuri na hapewi vile vitu vinavyohitajika huo unakuwa ni ubaguzi kwani uelewa wake na u unakuwa tofauti na uelewa wa watoto wengine"amesema Meena
Pia ameitaka serikali kuangalia mtaala kama ni jumuishi kwa makundi ya watoto wenye mahitaji maalumu.
Mtaala jumuishi ni ule ambao utawezesha wanafunzi wote kujifunza na walimu kuutekekeza kwa kuzingatia mahitaji halisi ya wanafunzi na utoaji wa elimu nyumbufu katika ngazi zote za elimu
Meena Wilberforce
Amesema dhana ya ujumuishi ni watu wote wanakua wanapata kitu kwa pamoja na si kwa baadhi ya makundi wapate na wengine wakose.
"Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 2014 pamoja na sheria ya elimu ya mwaka 1978 haihitaji moja kwa moja elimu jumuishi, Elimu jumuishi inatajwa zaidi katika Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 pamoja na sera ya taifa kuhusu huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu ya mwaka 2004"amesema Meena
Naye Afisa Elimu maalumu Dodoma jiji Msingi pamoja na sekondari Agnes Mwingira ameiomba Serikali iangalie namna bora ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu wanapofeli madarasa ya mitihani ya taifa kwani wengine wanakuwa wakirudia hata mara 3.
"Wanapopata fursa ya kufanya mitihani wa taifa anapata wastani wa D na kushindwa kuendelea na darasa lingine ifike pahala waone hiyo sera wanaiwekaje ili watoto waendelee kwasababu mi kuna siku niliwahi kuulizwa na mwanafunzi mwalimu mi ntazeekea hapa wanashindwa kutokana na changamoto waliyonayo "amesema Agness
Kwa upande wake mwalimu Joseph Degera kutoka shule maalum Dodoma viziwi amesema mfumo unaojadiliwa unahitaji vitu mbali mbali changamoto wanayoipata wao ni lugha ya alama na kusema katika kada ya elimu suala la lugha bado haijapewa kipaumbele.
"Tunawanawaomba wadau
wa elimu waendelee kupaza sauti kwa serikali kama wnavyopaza kwa vitu
vingine wakumbuke na suala la lugha ya alama katika kufundisha ili watoto
wapate mawasiliano"
0 Comments