📌MWANDISHI WETU
VIJANA
wanaojishugulisha na kilimo hai kwenye wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma
wameiomba serikali iwasaidie kupata uhakika wa masoko ya mazao yao ikiwemo
alizeti, mahindi, kunde, ufuta na mazao ya mboga mboga.
Wamaetoa ombi hilo
mwishoni mwa wiki wakati wataalam wa Wizara ya Kilimo wanaofanya ufuatiliaji wa
utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Vijana
kushiriki kwenye sekta ya Kilimo (NYSA) kuzalisha ajira walipotembelea vikundi sita vya vijana.
Tunalima mboga mboga mboga pia alizeti hapa kijijini lakini changamoto yetu imekuwa uhaba wa masoko ya mazao yetu hali inayopunguza morali ya vijana kuendelea na kazi za Kilimo
Christopher Joseph kijana mjasiliamali
Akizungumzia kuhusu
kazi zilizofanywa na shirika la Kilimo Endelevu (SAT) linalotekeleza mradi wa
Wanawake Dodoma katika Maendeleo ya Kilimo na Biashara (DWABI) Mratibu wake
Elizabet Kilia alisema jumla ya vijana 2,563 kati yao wasichana 2,354 na
wavulana 209 wamefikiwa na kuunganishwa kwenye vikundi vya kilimo hai (organic
farming).
Aliongeza kusema jumla
ya vikundi 90 katika wilaya za Chamwino, Mpwapwa na Dodoma wamefikiwa na elimu
ya kilimo hai na ujasiliamali kupitia shirika la SAT ambapo linalenga kuboresha
maisha ya vijana hususan akina mama wadogo (young mothers) kiuchumi kupitia
kilimo ambao wamezaa mapema wakiwa na umri mdogo .
Elizabet alisema kwa upande wa ujasiliamali jumla ya
vijana 1,900 wamejengewa uwezo kwenye ujasiliamali kwa nadharia na vitendo
kuweza kutengeneza bidhaa za kijasiliamali kama batiki, kuongeza thanani ya
zao la ubuyu, sabuni za maji na mikoba ya shanga,
Naye Mratibu wa Mkakati
wa Vijana Kushiriki katika Kilimo toka Wizara ya Kilimo aliyeongoza tumu ya
wataalam kukagua miradi ya Vijana Revelian Ngaiza aliwapongeza vijana wa
Chamwino kwa ubunifu wao uliokuza uzalishaji wa mazao hali ilisaidia
kubaidilisha maisha yao kwa kuwa na uhakika wa kipato kwenye kaya .
Ngaiza aliongeza kusema
suala la uhaba wa masoko kwa mazao ya kilimo ni agenda kuu ya serikali ya awamu
ya sita ambapo mikakati imewekwa ili kuwezesha wakulima wapate masoko na kuuza
mazao yao, hivyo amewataka vijana kutokata tamaa bali waendelee kujishughuli
kazi za kilimo ikiwemo za uongezaji thamani mazao ya kilimo na mifugo.
Rais Samia Suluhu Hassan tayari ameshatoa maagizo kwa wizara ya Kilimo na ile ya Viwanda na Biashara kuhakikisha mazao ya wakulima yanapata masoko ya uhakika .Agizo hilo alilotoa wakati akihutubua Bunge huvu karibuni, hivyo vijana endeleeni kulima kwa kuzingatia tija na soko litapatikana
Ngaiza.
Kuhusu changamoto ya
vijana kupata ardhi na kuondokana na gharama kubwa ya kukodi Ngaiza alitoa wito
kwa Halmashauri nchini kote kutenga ardhi maalum kwa ajili ya vijana kwenye
vijiji ili waweze kuzalisha mazao ya Kilimo na kuwa na uhakika wa ajira na
kipato hatua itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa Taifa kuhusu vijana
kushiriki kwenye sekta ya Kilimo.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa shirika la Kilimo Endelevu (SAT) Janet Maro alisema wapo tayari
kununua mazao yote ya vijana yaliyozalishwa kwa njia ya Kilimo hai msimu huu
ikiwemo alizeti, karanga, ufuta, mahindi na mpunga.
Katika kuhakikisha
vijana wanawezeshwa na kusimamiwa kuzalisha mazao kwa njia ya Kilimo hai SAT
tayari imefanikiwa kutoa mafunzo kwa maafisa ugani 40 toka wilaya za Chamwino
(19),Dodoma (1) na Mpwapwa (20) mafunzo yaliyotolewa kwenye kituo cha mafunzo
Vianzi mkoani Morogoro mwaka 2020.
👉Habari na picha na Wizara ya Kilimo
0 Comments