📌HAMIDA RAMADHANI
MAMALAKA ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imesema, ujio wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), umeleta
mabadiliko makubwa katika tasnia ya habari bila kusahau haki za msingi za
binadamu.
Pia, TCRA imewataka wananchi
wote, kuhakikisha wanaweka nywila ‘password’ kwenye simu zao na kutokubali
kumwonyesha hata mwenza wake kwani ni hatari.
Hayo yamebainishwa leo Jumanne,
tarehe 11 Mei 2021 na Dk. Philip Filikunjombe, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi
na Utekelezaji wa Sheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi na wahariri wa habari wa mtandaoni, mkoani Morogoro, iliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),Dk. Filikunjombe amesema, Tehama imeleta mabadiliko katika dunia ya sasa ambapo, dunia imekuwa kijiji kwa kuongeza kwa watumishi wa mtandao huku kasi ya mtandao kuwa ya kasi kubwa.
Ni ukweli usiopingika, tumetoka kwenye matumizi ya kizamani na sasa tupo katika mitandao ya kijamii ambapo huko tunapata habari zetu kwa rahisi na haraka zaidi
Dk.
Filikunjombe.
Aidha ametoa rai kwa watumishi wa
mawasiliano kwanjia ya mtandao kuweka nywila (Password) ikiwemo kwenye
simu zao, ili taarifa zao ziwe na usiri ili kuepuka wadukuzi.
Amesema, suala la kuweka nywila,
haijalishi kama uko kwenye mahusiano ikiwemo ndao kwani Kanuni za Maudhui ya
Mtandaoni za mwaka 2020, zinataka kila mmoja awe na nywila yake mwenyewe pasina
mtu mwingine kuijua.
Dk. Filikunjombe amesema,
kutokana na mjadala wa uwepo wa wadau mbalimbali kutaka maboresho ya kanuni
hizo hivyo, TCRA imeanza kupokea maoni ya wadau ili ziweze kuboreshwa.
Amesmea, kila mmoja, ajitokeze
kutoa maoni yake kwa kuangalia ni eneo gani linahitaji maboresho zaidi
yatakayozifanya kanuni hizo kuwa rafiki kwa watumiaji wote.
0 Comments