📌NTEGHENJW HOSSEAH, OR-TAMISEMI
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Prof. Riziki Shemdoe amesema uhamisho wa watumishi wa Tawala
za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa utafanyika mara nne kwa mwaka yaani
kila robo ya mwaka husika.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Prof.
Shemdoe amesema kila tarehe 10 ya mwezi
unaofuata baada ya robo mwaka kwisha uhamisho utafanyika na majina yatawekwa
kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI.
Robo kwanza ya mwaka yaan Julai - Septemba majina ya uhamisho yatakua yanatoka tarehe 10 October , na robo ya Pili Oktoba - Desemba majina ya uhamisho yatatoka Januari 10.
Aliongeza kuwa: " katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka
April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai
10."
Aidha Prof.Shemdoe
amebainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaohamishwa yatawekwa
kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
Pia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini
kuwasilisha orodha ya watumishi wa kuhama
ofisi ya Rais-TAMISEMI kila tarehe 05 ya mwezi unaofuata baada ya robo
mwaka.
Aidha, amewata Makatibu Tawala wote kutokupitisha
maombi ya watumishi wanaotaka kuhamia kwenye majiji, manispaa na miji kwa kuwa
maeneo hayo yana idadi kubwa ya watumishi.
Aidha, Profesa Shemdoe aliwataka Makatibu Tawala
kuwapa kipaumbele watumishi wenye changamoto
mbalimbali zilizothibitishwa.
Prof.Shemdoe ametoa wito kwa watumishi wote kubaki
kwenye vituo vyao na barua za uhamisho
zitatumwa kwa waajiri wao na wataona majina yao kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais
TAMISEMI.
Pia amewataka watumishi kujihadhari na matapeli
wanaotaka fedha kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wao kwa kuwa Uhamisho ni bure
na ni haki ya kila mtumishi.
Amesema kuwa Barua za Uhamisho za kipindi cha nyuma
ambazo zilishafika Ofisi ya Rasi TAMISEMI zinashughulikiwa na majina yatatolewa kila mwezi mpaka Juni 30
kabla utaratibu mpya haujaanza kutumika
0 Comments