📌MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Mohamed Mchengerwa
amewaonya wakuu wa Taasisi za umma nchini wenye lengo la kujitoa katika
matumizi ya mifumo iliyotengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na
kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria
Mhe.Mchengerwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kutembelea ofisi hiyo na kuzungumza na
watumishi wa Mamlaka hiyo ya Serikali Mtandao
''Ninafahamu kuna baadhi ya Taasisi za Serikali kushirikiana na wadau wao
wanaotaka kujitoa katika matumizi ya mifumo inayotengenezwa na eGA,kujitoa
katika mifumo ambayo tayari tumeirasimisha kwa misingi ya sheria ya Serikali
Mtandao namba 10 ya mwaka 2019 na kanuni zake za mwaka 2020 ni kinyume cha
Sheria''Alisema Waziri wa Mchengerwa
Nitoe rai na onyo kwa wakuu wote wa Taasisi za Serikali kuwa hakuna Taasisi wala Ofisi yoyote ya Serikali ambayo inaruhusiwa kujitoa kwenye mifumoinayosimamiwa na eGA
Waziri Mchengerwa
Aidha pia ameiagiza eGA kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wanadhibiti uvujaji wa siri lakini pia utolewaji wa taarifa ambazo hazistahili kwenda moja kwa moja kwa watumiaji wa kawaida
Vile vile ameipongeza eGA kwa jitihada kubwa wanazofanya za kuendelea kubuni mifumo ambayo ina rahisisha utendaji kazi Serikalini ambapo pia amewasihi kuendelea kutekeleza jukumu hilo kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Mhandisi Benedict Ndomba yeye ametaja baadhi ya athari zinazoweza kujitokeza endapo Taasisi za umma hazitopeleka taarifa za mifumo inayoanzisha kuwa ni pamoja na kutokufata viwango na miongozo jambo linalopelekea mifumo kutowasiliana
0 Comments