📌ANGELA MSIMBIRA-TAMISEMI
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Prof. Riziki
Shemdoe amesema kuwa shule ya Sekondari ya Kibasila ni miongoni
mwa shule 86 zilizokarabatiwa kupitia
mradi wa lipa kulingana na Matokeo
unaolenga kuoboresha mazingira ya
kufundisha na kujifnzia kote nchini
Prof. Shemdoe ameyasema hayo leo kwenye hafla ya
uzinduzi wa magari 184 kwa ajili ya ufuatiliaji katika shule za Msingi kwenye
Halmashauri zote nchini iliyofanyika
katika shule ya sekondari ya kibasila Mkoani Dar es salaam.
Akifafanua kwanini walichagua uzinduzi wa magari
ufanyiwe hapo amesema kuwa shule ya
Sekondari ya Kibasila ilijengwa mwaka
1951 na kuanza kutumika kama sekondari mwaka 1979 na ni moja ya shule ambayo
imekarabatiwa kupitia mradi wa lipa
kulingana na matokeo
Amefafanua kuwa lengo kuu la kuchagua eneo hilo ni kuonyesha juhudi kubwa iliyofanywa na
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuboresha miundombinu ya shule
ikiwemo ukarabati wa shule kongwe.
Amesema kuwa pia eneo la uzinduzi limepambwa na mjasiriamali mmoja
wa wanufaika wa nikopo ya asilimia kumi
inayotolewa na Serikali katika Manispaa ya Temeke hii inaonyesha utekelezaji wa
Sheria unaofanywa na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuhakikisha wananchi
wanajikwamua kiuchumi.
Amesema
pamoja uzinduzi wa magari pia
kuna ukarabati wa shule umefanywa kwa
ajili ya kuhakikisha wanafunzi wa Kitanzania wanapata mazingira mazuri ya
kujfunzia.
0 Comments