📌HAPPINESS MTWEVE
SERIKALI imeitaka Shirika la Umeme nchini(TANESCO)
na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wanakamilisha upanuzi wa kituo
cha kupoza umeme cha kV 220/33 katika Kituo cha kufua umeme cha Mtera kabla ya
Oktoba mwaka huu utakaogharimu Sh.bilioni 7.8.
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ametoa
agizo hilo jijini Dodoma alipofanya ziara katika kituo cha kufua cha umeme cha
Mtera kilichopo kati ya Mkoa wa Iringa na Dodoma ambapo alikagua sehemu ya
Bwala la Maji la Mtera.
Pia amekagua mitambo ya uzalishaji umeme na
maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho kipya cha kupoza umeme, mgodi unapozalisha
umeme, sehemu inayotoa Umeme kupeleka kwa watumiaji.
Byabato amesema serikali inafanya upanuzi wa Kituo hicho cha kupoza umeme ili kuongeza uzalishaji wa Umeme ambapo kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kusambaza Umeme katika mkoa wa Iringa na Dodoma.
Amebainisha kuwa kazi hiyo ya upanuzi ilichelewa
kutokana na masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa vifaa vya umeme kutoka
nje ya nchi, na mkandarasi kuamua kuondoka ili kusubiri vifaa hivyo, sasa
serikali imeagiza arejee haraka nchini na kuanza kazi hiyo itakayofanyika usiku
na mchana ili iweze kukamilika kwa wakati.
0 Comments