SERIKALI KUENDELEA BORESHA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIARA

 


📌RHODA SIMBA

SERIKALI kupitia Wizara ya  viwanda na  biashara imesema inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara nchini ili kuwafanya wajasiriamali  wafanye kazi kwa  ufasaha kwaajili ya kujikwamua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa taifa. 

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Exaud Kigahe wakati akifungua kongamano la chama cha wafanyabiashara wanawake Tanzania,Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC).

Aidha lengo la kongamano hilo ni kuwapa nafasi wafanyabiashara kujifunza, kubadilishana mawazo,uzoefu katika biashara tofauti  ambazo kila mmoja anafanya. 

Leo ikiwa ni siku ya mama duniani niwapongeze sana kwa kongamano lenu,mtumie fursa hii kuzalisha biashara zenye viwango,kwa maana Tanzania siyo kisiwa  unapoingia hapa utakutana na bidhaa mbalimbali
 Kigahe

Amesema kupitia wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha hasa ,katika fursa zinazojitokeza katika miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

"Zipo fursa mbali mbali kuna miradi mikubwa ya  bomba la mafuta,SGR fungueni makampuni ili muendelee kutumia fursa hizi,kwa maana juhudi za kuhaikisha wanawake wanawezeshwa zitaendelea tunaamini ya kwamba ukimuwezesha mwanamke umewezesha jamii na nimpongeze tu mama yetu Rais Mama Samia Suluhu Hassan anaendelea kufungua milango ya biashara"amesema Kigahe

Naye Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe.Antony Mavunde amewataka wakina mama  wasiwe watazamaji wa fursa zinazojiteza  kwani kwa sasa Dodoma  limekua jiji ambalo kuna fursa mbali mbali za kimaendeleo.

Sisi tunatoa mikopo,hadi milion kumi,natamani kina mama wachangamkie hii fursa na  kama mtu haoni akichukua mkopo atafanyia nini jamani niwatake kina mama wajikite katika zoezi la uchakataji wa zabibu naamini ni soko zuri na linalipa haswa

Mavunde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho cha  TWCC, Kapesi Oneya amesema lengo hasa la kongamano hilo ni kwaajili ya siku ya mama duniani,ili wafanye malengo fursa lakini wengine hata kukitambua chama  hicho ni nini na kina fanya nini.

"Chama chetu kina wanachama 6000  ambao ni wajasiriamali lakini hapa kwa mkoa wa Dodoma kina wajasiriamali 250 leo tupo hapa kwaajili ya mafunzo,kujuana,waelewe nini cha kufanya wanatakiwa wafanye nini kutoka biashara ndogo kwenda  biashara ya kati"

Na kuongeza kusema kuwa "Watawezeshwa kwa mafunzo utaratibu wa kuboresha biashara atakapochukua mkopo kuna baadhi ya taasisi  za kifedha  zinatoa mikopo kwa riba kubwa na namna ya kufanya"amesema Kapesi

Catherine Chekani ni moja kati ya washiriki wa kongamano hilo ambapo amewataka kina mama kina  waache kujiita wamama wa nyumbani kwani hata kama anafanya shughuli ya kuuza maandazi huyu ni mjasirimali si mama wa nyumbani.

Kuna wakati tunachoka tunavyotoka out kama hivi tunafamiana na kutambua baadhi ya bidhaa ambazo zinauzwa na wenzetu tunabadilishana uzoefu kwakweli niseme nafurahi san kwa siku ya leo.

Naye mshiriki Khadija Hassani amesema kupitia kongamano hilo wao kama wanawake  wana amini wataenda kutoka na vitu vipya,vya kwenda kuvifanya watakapoenda kwenye shughuli zao za ujasiriamali.

 

Post a Comment

0 Comments