📌ALEX
SONNA
MAMLAKA
ya udhibiti wa huduma za nishati na maji hapa nchini UWURA leo Mei 11, 2021
imezindua ripoti ya tathmini ya hali ya utendaji kazi na utoaji huduma kwa
mamlaka za maji hapa nchini ripoti inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma za
maji kwa wananchi.
Akizindua
ripoti hiyo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
amewataka watendaji katika mamlaka zote za maji ngazi zote hapa nchini kufanya
kazi kwa kutanguliza uzalendo, uadilifu na weredi katika kazi zao.
Amesema Serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha huduma ya maji inawafikia wananchi kama inavyotakiwa lakini kuna baadhi ya watendaji hawatimizi majukumu yao vizuri.
Serikali inatumia fedha nyingi sana katika kutekeleza miradi lakini miradi hiyo haifanyi kazi kwa uzembe wa watendaji katika kusimamia miradi hiyo, nataka kila mmoja afanye kazi kwa weredi mkubwa ili wananchi wapate huduma za maji
Mhe. Majaliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amezitaka mamlaka za maji kwenda kusimamia ipasavyo
ukusanyaji wa ankara za maji ili kuwezesha mamlaka hizo kuendelea kujiendesha
bila hasara huku zikizingatia sheria bila kuwabambikizia Ankara watumiaji wa
maji kwani kuna malalamiko mengi sana.
Ameongeza
kuwa “mkahamasishe watu kulipa ankara za maji na h ii sio kwa wananchi tu hata
kwenye taasisi za serikali zote zilipe bili yeyote anayetumia maji lazima alipe
ankara za maji mkasimamie hilo, pia tumepiga marufuku ukataji wa maji siku za
wikendi au siku kuelekea wikendi” amesema.
Aidha
ameitaka EWURA kwenda kusimamia uboreshwaji wa huduma za maji na kujenga
utaratibu wa kufuatilia uboreshaji wa sera na kanuni katika kuhakikisha
wananchi wanapata huduma bora za maji ipasavyo na kufuatilia tatizo la ucheleweshwaji
wa miradi ya maji.
Awali, Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amesema wao kama Wizara watahakikisha wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji na hawatamvumilia mtu yeyote atakayekwenda na kutaka kurudisha nyuma jitihada hizo.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje akitoa
taarifa kuhusu ripoti hiyo amesema ripoti hiyo itasaidia katika kuimarisha
utendaji kazi kwa Mamlaka zote na watakuwa wakitoa ripoti ya tathmini
iliyofanyika ya utendaji wa kila Mamlaka katika mamlaka za Mikoa na miradi ya
kitaifa na mamlaka za miji midogo na Wilaya.
Amesema
wamefanya tathmini ya utendaji wa kila mamlaka na kupata Mamlaka zilizofanya
vizuri katika kutoa huduma katika makundi ambapo kwa kundi la usimamizi wa
miradi ya kitaifa aliyeibuka mshindi ni KASHWASA, Mamlaka za Mikoa ni Mamlaka
ya Mkoa wa Moshi na Mamlaka za miji na Wilaya ni Bihalamuro ambazo zimezawadiwa
shilingi milioni 21 kila mmoja ambazo watazitumia katika kununua dira za maji.
0 Comments