📌HAPPINESS MTWEVE
RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya Sikukuu ya
Eid ul-Fitr kwenye kituo cha makao ya Taifa ya kulelea watoto wanaoishi kwenye
mazingira magumu na hatarishi kinachomilikiwa na Serikali kupitia Idara kuu ya
Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto.
Zawadi hiyo imekabidhiwa leo Mei 10 mwaka huu, kwa
uongozi wa kituo hicho kilichopo eneo la Kikombo jijini hapa kwa niaba ya Rais
Samia na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mwanaidi Ali Khamis muda mfupi baada ya
kuzindua Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Idara hiyo ya Maendeleo ya Jamii.
Naibu waziri huyo alisema rais ametoa zawadi ya mchele, mafuta na kitowewo ambao ni mbuzi wawili kwa ajili ya kushiriki pamoja na Watoto hao katika sikuu hiyo ambayo ni siku ya furaha baada ya waumini wa duni ya kiislamu kukamilisha nfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani.
Rais amenituma salaam nyingi amesema niwambia anawapenda na serikali inawajali ana na ndio mana imeendelea kuwakumbuka hata katika siku na matukio muhimu kama hili la sikukuu ya Eid ul- fitr.
Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis
Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo Ofisa
Mfawidhi wa makao ya hayo, Tulo Masanja amesema wamepokea kwa moyo wa Shukrani
zawadi hizo na kwa niaba ya watoto anamshukuru, Rais Samia kwa upendo wake mkuu
kwa watoto hao.
Masanja ameeleza kuwa kituo hicho ni kituo Cha mfano, kina jumla ya watoto 28 wakike 16 na wakiume 12 ambapo wanapatiwa huduma ya malazi, chakula, mavazi na elimu na kwamba wamehamishwa kutoka kituo na kurasini jijini Dar es Salaam.
Amesema kituo hicho ambacho ni uwekezaji mkubwa
uliofanywa na serikali kina uwezo wa kuchukua watoto 250, kuna kituo cha
kulelea watoto wadogo(day care) wapatao 60, ukumbi wa mikutano, Zahanati, bwalo
la chakula, mabweni, kalakana, viwanja vya michezo, maktaba n.k.
Masanja amesema jukumu la serikali ni kuhakikisha
watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi linakoma na jitihada moja
wapo ni pamoja na uwekezaji huo mkubwa uliofanywa, licha ya kuwa nia si
kukusanya watoto na kujaza vituo ila lengo ni kuwakusanya kuwahudumia na
baadaye kuwarejesha katika jamii, wazazi na walezi wao.
0 Comments