📌HAPPINESS MTWEVE
WAZIRI wa Kilimo, Profesa Adolf Mkenda
amewaagiza wakala wa mbegu Bora za
kilimo nchini(ASA) kuhakikisha wanafufua mashamba yote 13 ya uzalishaji wa
mbegu ambayo yamegeuzwa kuwa mapori.
Amesema endapo mashamba hayo yatafufuliwa na
kuendelea na uzalishaji wa mbegu wenye tija itasaidia kuipinguzia serikali
mzigo na gharama ya kununua na kuagiza mbegu nje ya nchi.
Profesa Mkenda ametoa agizo hilo jijini Dodoma leo
wakati akizungumza na wajumbe wa bodi na Menejimenti ya ASA iliyoambatana na
utoaji wa vyeti vya shukrani kwa wajumbe wa bodi wanaomaliza muda wake.
Waziri amefafanua kuwa itakuwa ni ajabu kuzuia
wananchi kuvamia mashamba hayo na kuyatumia wakati mashamba hayo yamekaa tu
hayatumiki na kuwa kama yametelekezwa.
Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ASA
Mwenyekiti wa bodi ya ASA Dk.Ashura Kihupi amesema wanakabiliwa na ufinyi wa
bajeti hivyo kushindwa kuendeleza mashamba hayo hivyo kujikuta wakiyaacha bila
kuyatumia na kuwa mapori.
"Gharama za kuendesha mashamba hayo ni kubwa
ikiwemo vitendea kazi na rasilimali watu ya kutosha, kwa Sasa tuna watumishi
150 huku mahitaji yakiwa 204, idadi hiyo haitoshi,"amesema Ashura.
Kuhusu agizo la waziri la kufufua mashamba amesema ASA
peke yake hawataweza kwani kwasasa mashamba yanayotumika ni 8 tu kati ya 13
yaliyopo, kwa kuwabserikali itaingilia Kati tunaamini itaongeza bajeti ili
kufanikisha hilo na mashamba mengine watayakodisha kwa wawekezaji hivyo kufanya
mashamba yote kufufuliwa.
0 Comments