📌JOHN BANDA
MBUNGE wa jimbo la
Bahi mkoani Dodoma Kenneth Nollo (CCM) amewashauri viongozi wa Chama hicho na
wale wa Serikali wilayani humo kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waendelee
kufanya kazi za maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati
Pia amesema katika
wilaya hiyo kuna upungufu wa zahanati 16 ambapo ifikapo mwaka 2025 atahakikisha
zahanati 10 zinakamilika ili kuwasogezea huduma za kiafya wananchi wanaoishi
katika kata za wilaya hiyo
Mbunge huyo aliyasema
hayo mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi mdogo wa nafasi ya katibu wa itikadi
na uenezi wa chama hicho wilayani bahi uliofanyika baada ya aliyekuwa
akiishikilia kuchaguliwa udiwani kata ya chali na baadae kuchaguliwa kuwa
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri, ambapo Nasson Kachinda aliibuka mshindi
Nollo alisema ili
kuhalakisha maendeleo ya wilaya hiyo ni vizuri kuwe na ushirikiano kati ya
viongozi wa CCM na wananchi ili kuweza kuibua kero zilizopo ili iwe rahisi
kuzifikisha serikalini ambako zitafanyiwa kazi kwa ajili ya maendeleo ya wilaya
hiyo
Viongozi wa chama mkishirikiana vizuri na wananchi mtaibua kero nyingi na zenye tija ambazo zikifikishwa na kufanyiwa kazi serikalini wilaya yetu itapaa kimaendeleo
Aidha aliwataka
viongozi kuendelea kuwahamasisha wananchi ili waendelee kujitolea kwenye kazi
za maendeleo na hasa nguvu kazi kwenye ujenzi wa zahanati ambazo yeye kama
mbunge wao pamoja na wadau wengine wamekuwa wakitoa mifuko ya sumenti kwa ajili
ya ujenzi
Katibu wa Itikadi na Uenezi Wilaya ya Bahi
Nasson Kachinda akiozungumza
jambo mara baada ya kuchaguliwa kushika nafasi
hiyo.
Alisema kwa upande wa
serikali mpaka sasa imeshatoa million 150 kwa ajili ya kumalizia ujenzi
wa zahanati za Chikopelo, Mayamaya na Mkakatika ambako wananchi walitolea nguvu
kwa kwa bidi kubwa
“viongozi endeleeni
kuwahamasisha wananchi waendelee kujitolea nguvu zao kwa kufanya kazi za
maendeleo, hasa kukusanya mawe na mchanga pamoja na kuchimba misingi ili
zahanati zijengwe
Naishukuru serikali
ambayo kutokana na maendeleo mazuri ya ujenzi wa zahanati za chikopelo,
Mkakatika na mayamaya wameshatoa million 150 inayogawanywa kwenda kumalizia
zahanati hizo tatu”, alisema Nollo
Aliongeza kuwa mpaka
sasa kupitia mfuko wa jimbo tayari ameshato million 30 kwa ajili ya ujenzi wa
zahanati za Nguji, njinia, na chikopelo ambapo ifikapo mwaka 2025 atakuwa
amekamilisha 10 kati ya 16 zinazohitaji
Mwenyekiti wa CCM
wilayani bahi Stewart Masima akiongea katika uchaguzi huo alisema tangu amekuwa
mwenyekiti hajawahi kupokea msaada toka kwa mbunge ambapo hata gari la chama
walikuwa wanaliogopa kulitumia kutokana na matairi yake kuwa vipara lakini
mbunge amesha nunua yote manne na gari limeanza kutumika
0 Comments