📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya kilimo,Mifugo na
Maji imetembelea miradi mikubwa ya maji ya Mzakwe na Buigiri iliyopo
jijini Dodoma huku ikiridhishwa na mwendelezo wa utekelezaji wa
miradi hiyo.
Akizungumza katika ziara hiyo Mei
4,2021 ,Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya kilimo,Mifugo na Maji Christina
Ishengoma ameipongeza Wizara ya Maji kwa kuendelea kutekeleza miradi hiyo
kwa ufasaha.
Baada ya kuzunguka na kuona visima vinajengwa baada ya muda tatizo la maji litapungua ,kwa hiyo baada ya mwaka mmoja tutaweza kupata maji ya kutosha katika jiji letu la Dodoma kwa kweli ninaashukuru sana wizara ya Maji kwa kushirikiana na DUWASA katika utekelezaji wa miradi hii
Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso takriban visima 10 vimechimbwa katika jiji la Dodoma huku mkakati wa maji kutoka ziwa Victoria ukiendelea.
“Watu katika jiji la
Dodoma wameongezeka Mhe.Rais ametupatia Bilioni 5 kuhakikisha tunafanya
maboresho ya haraka ,tumechimba visima takriban 10 ,kuna visima vikubwa
3 ambavyo tumevichimba kimoja kina uwezo wa kutoa zaidi ya lita 400,000
kwa saa tuna tank kubwa hapa Buigiri la lita milioni 2.5 hii
yote kuhakikisha wananchi wa Dodoma wanapata maji kwa haraka na
mkakati wa haraka tulionao ni kuleta maji kutoka ziwa Victoria”amesema.
Kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira jijini Dodoma Mhandisi Aron Joseph amesema mradi wa maji Buigiri Chamwino umefikia asilimia 98 .
"Kama DUWASA tunahakikisha huduma ya maji inaboreka zaidi katika jiji la Dodoma , mradi huu wa Buigiri Chamwino ulikuwa wa thamani ya Tsh.bilioni 2.5 lakini tumeutekeleza kwa Tsh.Milioni 998 kwa maelekezo ya wizara katika kuhakikisha tunapunguza gharama na tumefanikisha kwa sababu tupo asilimia 98 ya utekelezaji wa mradi ili uweze kukamilika." amesema.
Hata hivyo, Kamati ya kudumu ya Bunge ya
kilimo,Mifugo na Maji imeishauri Wizara pamoja na taasisi zake ikiwemo mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira jiji la Dodoma [DUWASA] na jiji la
Dodoma kwa ujumla kuwa na mpango kabambe wa kutoa elimu kwa wananchi namna ya
kujenga nyumba zitakazokuwa zina miundombinu ya kuvuna maji ya mvua kwa wingi
ili kuondoa changamoto ya uhaba wa maji .
0 Comments