📌ANGELA MSIMBIRA- TAMISEMI
KAMATI ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa
imeshauri Serikali kudhibiti madalali katika upatikanaji wa vizimba na
ushushaji wa mizigo katika soko la kisasa la Ndugai jijini Dodoma.
Kamati imetoa ushauri huo mara baada ya ziara ya Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa walipotembelea soko la Ndugai
kuangalia hali ya utoaji wa huduma Katika soko hilo ambalo limejengwa na
Serikali kwa gharama ya Sh bilioni 14.6.
Akizungumza katika ziara hiyo Mbunge wa Hai Mhe.
Saasisha Mafuwe amesema kushindwa kuimarika kwa biashara katika soko hilo
kunatokana na madalali kuhodhi vizimba sambamba na kuzuia magari ya mizigo
kushusha hapo.
Aidha akichangia hoja katika Soko hilo hMbunge wa
Viti Maalum(CCM) Balozi Pindi Chana amewataka wataalam kuahkikisha wanafanya
utafiti wa kupata takwimu sahihi ya wafanyabiashara wanaotumia soko hilo na
kuwahamasaisha wananchi kujenga katika
eneo hilo ili Soko liweze kuchangamka na kuwavutia wananchi kuja kununua bidhaa
katika Soko hilo.
Akihitimisha katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa
Kamati Mhe. Chaurembo kusema kuwa miradi
ya ujenzi wa masoko katika Halmashauri izingatie mahitaji ya wananchi kwa kuwa
mengi hujengwa kwenye maeneo ambayo uendeshaji wake umekua mgumu na kufanya
miradi hiyo kutokuingiza mapato kwa Serikali.
Mhe. Abdallah Chaurembo ameshauri kuhakikisha mikakati endelevu ya kutoa elimu kwa jamii
inawekwa ili kuwajengea wananchi uelewa kuhusu matumizi ya masoko nchini
Wananchi wengi wamekuwa wakiogopa kuingia kwenye masoko yaliyojengwa kwa kuhofia gharama ya vitu kuwa kubwa hivyo Serikali iweke mikakati ya kutoa elimu ili kuondoa dhana hiyo
Mhe. Chaurembo.
Akijibu hoja za Wabunge Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu ameieleza Kamati kuwa
watahakikisha wanafanya mapitio ya
mpango wa biashara wa soko la Ndungai
ili uendane na kile
kilichokusudiwa.
Mhe. Ummy amefafanua kuwa ili kuweza kurejesha uwekezaji wa shilingi bilioni 14.6 kuna haja ya kupitia mpango wa biashara wa kuanzishwa kwa soko hilo ili isiende kinyume na matarajio yaliyopangwa awali.
Mhe. Ummy amesema
kuwa Serikali itakuja na mkakati wa kutekeleza maoni na ushauri walioutoa wajumbe wa kamati hiyo
ambao utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika Soko hilo la Kisasa.
Mradi wa Soko la Ndigai ulibuniwa kwa kuangalia (Long time plan) kwa kuwa Dodoma imekuwa ni Makao Makuu ya Nchi, lakini pia ongezeko la watu , hivyo ni kweli zimewekwa shilingi bilioni 14.6 lakini ukiangalia makisio ya marejesho kiasi hicho cha Fedha kitarudi
Waziri Ummy
Amesema kuwa kwa mwaka ilikadiriwa kupata kiasi cha shilingi bilioni 1.8
hivyo kwa muda wa miaka 15 itawezekana kupata shilingi bilioni 27 na
tangu soko limeanza kufanya kazi tayari wameshakusanya kiasi cha shilingi milioni
100 hivyo mpango wa muda mrefu utalipa.
Mhe. Ummy amesema kuwa viwanja vingi vya makazi
vimetengwa mtumba , nzuguni , Chamwino ambapo bado hapajajengwa hivyo
wanategemea mara baada ya watu kujenga watakuwa wakitumia soko hilo kupata
huduma za mahitaji mbalimbali ya kijamii.
Aidha Ameuelekeza
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
kuhakikisha wanapitia mpango wa biashara wa
Soko la Ndugai ili liendane na
uhalisia wa awali nini kilikuwa kimekusudiwa katika soko hilo.
Aidha amewagiza Halmashauri ya Jiji la Dodoma
kuhakikisha wanawaondoa madalali katika soko hilo kwa kufanya utafiti wa kina wamiliki wa vizimba ili kuwa na wamiliki halali wa maeneo yao.
0 Comments