📌PENDO MANGALA
JUKWAA la Asasi za Kiraia Nchini limekutana Jijini Dodoma kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG ya Mwaka wa Fedha 2019/2020 lengo likiwa ni kuweza kupata uchambuzi wa Taarifa hiyo na kuweza kuchukua hatua ili kuboresha uwajibikaji,uwazi katika kuboresha utendaji kwa Serikali za Mitaa na Serikali kuu.
Akizungumza Jana Jijini hapa katika ufunguzi wa mkutano wa jukwaa hilo Mkurugenzi Mkuu wa Asasi ya Kiraia ya Foundation for Civil society,(FCS) Francis Kiwanga amesema Mkutano wa Jukwaaa hilo ambalo limeshirikisha Wadau mbalimbali umebaini kuwa utekelezaji wa miradi bado kuna changamoto.
Tunashukuru Sana kwa kuwa Serikali imekuwa ikitupa ushirikiano pale tunapohitaji,Pamoja na hayo jamii imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inatupa ushirikiano na kutupa urahisi wa kutimiza majukumu yetu Kama asasi za Kiraia.
Francis Kiwanga
Mbali na hayo ameeleza kuwa kwa kuona umuhimu wa maendeleo kwa jamii ,asilimia 15 ya AZAKI zinawajibika Katika ufuatiliaji wa miradi ya maji nchini ili kuwasukuma watendaji kuwa wabunifu Katika kutatua kero kubwa ya Uhaba wa maji nchini.
Kilio kikubwa kwa Wananchi hususani wanawake ni maji,asilimia 35 ya miradi ya maji nchini imetumia pesa nyingi lakini haijakamilika na ikitokea imekamilika basi haitoi maji, hali hii inapaswa kuangaliwa upya ili kuisaidia Serikali kutopoteza fedha kwa matumizi yasiyo na tija.
Francis Kiwanga
Licha ya hayo amesema kuwa ili AZAKI hizo ziweze kufanikiwa,ushirikishwaji wa Wananchi Katika maeneo yote unahitajika ili kuongeza muda mwingi nguvu Katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo.
Tutachukua maoni
ya Wana AZAKI na kuyafanyia kazi,tunatarajia kuona kila miradi ya maendeleo
iliyopo kwenye jamii inafanikiwa ,"alisisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu Ludovick Utouh ambaye pia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu amesema Taasisi yake imefanya uchambuzi wa Ripoti hiyo na kubainisha kuwa Mashirika ya umma yanapokosa wakurugenzi wa bodi panakuwa na changamoto katika utendaji.
SOMA HII PIA👉👉👉CHINA YAIPATIA SH. BILIONI 35.37 KWA AJILI UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO
0 Comments