📌RHODA SIMBA
JAMII imeaswa kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu ndani na badala yake wametakiwa kutoa fursa ya elimu kwa watoto hao kama walivyo watoto wengine wasio na ulemavu.
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Meneja wa mradi wa Elimu Jumuishi, Suleiman Ibrahim mradi unaofadhiliwa na kanisa la Free Pentecoste na information center on disabilities, katika Warsha ilio wakutanisha wadau,kamati ya kulea baraza la watoto pamoja na kikundi cha wazazi.
Aidha amesema Lengo la warsha hiyo ni kuwaleta wadau muhimu wa elimu jumuishi ili waweze kubainisha majukumu yao na kuona namna bora ya kutekeleza ili kufikia lengo la upatikanaji wa fursa ya elimu bora kwa watoto wenye mahitaji maalumu ya kielimu.
Amesema katika kuwaongezea fursa watoto wenye ulemavu mradi umekua ukifanya shughuli mbalimbali za kuona namna gani miundo mbinu rafiki katika shule za mfano zinapatikana, pamoja na kutoa mafunzo kwa walimu ili kujua mbinu bora za ufundishaji.
Lakini pia tunatoa mafunzo kwa walimu ili kujua namna ya upimaji wa watoto wenye mahitaji maalumu,kuwawezesha walimu kubaini changamoto za watoto na kutoa rufaa stahiki
Na kuongeza kusema kuwa,"kupamnana kujenga vyoo rafiki kwaajili ya watoto wenye ulemavu,kutoa elimu na mafunzo juu ya masuala ya sheria na sera kuhusu watu wenye ulemavu,kutoa elimu na mafunzo juu ya haki za za watoto wenye ulemavu"amesema Ibrahim.
Sambamba na hayo amesema malengo mengine ni pamoja na kutoa vifaa visaidizi vya kufundishia na kujifunzia kwaajili ya watoto wenye ulemavu,kuendeleza harakati za ushawishi na utetezi ili kupata sera madhubuti ambayo itaeleeza bayana elimu jumuishi.
"Lakini pia tunajikita katika kuendeleza harakati za ushawishi ili kupata mtaalamu rafiki wa watoto wenye mahitaji maalumu,kufanya utetezi kwaajili ya kuongezewa fursa ya elimu kwa watoto wenye ulemavu,
"tunafanya utetezi juu ya
kuongezewa kwa nafasi za watu wenye ulemavu katika utoaji wa maamuzi ndani ya
jamii,kuendesha shughuli za halaiki ili kukuza uelewa wa jamii kuhusu
masuala ya ulemavu ili kupunguza mtazamo hasi"amesema Ibrahim
Pamoja na hayo amesema wao kama mradi wanaunda vikundi na kuvijengea uwezo ili kuwa sauti ya pamoja na katika kudai haki za watu wenye ulemavu na mafunzo ya viongozi wa serikali za mtaa na Halmashauri.
0 Comments