📌HAMIDA RAMADHANI
JAJI Mstaafu Justice Makaramba
amesema, wanahabari wengi wamekuwa wakikumbwa na vitisho na manyanyaso pindi
wanapokuwa katika majukumu ya kila siku kazini.
Pia, amesema kumekuwa na kasumba
nyingine ya waandishi wa habari kesi zao kutofatiliwa mahakamani kwa dhana
ya kuwashitaki watu wasio julikana.
Amebainisha hayo leo Jumatano,
tarehe 12 Mei 2021 na Jaji Makaramba wakati akiwasilisha mada ya mifumo ya
kikanda na kimataifa ya kuhakikisha usalama wa wanahabari katika mafunzo
yalioandaliwa na Mtandao wa Utetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC Mkoani
Morogoro.
Aidha ameyataja matukio mabaya
yanayowakumba waandishi kuwa ni pamoja na kuuawa, kutekwanyara, kupotea,
kuwekea kizuizini huku akisisitiza matukio hayo huwakumba waandishi wanaoandika
habari hususan za uchunguzi au kuigusa hasa serikali.
Hata hivyo, amesema kwa Mujibu wa
Takwimu ilizotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), zinasema kuanzia mwaka 2018 mpaka 2019 kulikuwa na matukio
156 ya kuuawa kwa waandishi duniani.
Hii inamaanisha kila ndani ya siku nne, mauaji ya mwandishi yanatokea na mauaji mengi yamekuwa yakitokea kwenye nchi ambazo hazina vita, nchi ambazo zimejaa na amani na utulivu wa kutosha
Jaji Mstaafu Makaramba.
Jaji huyo amesema, kazi ya
mwandishi ni pamoja na kuihabarisha jamii kuhusu masuala mbalimbali.
SABABU 3 WAANDISHI
KUWA SALAMA.
Jiji Mkaramba amezitaja kuwa
1: Ili aweze kufanya kazi
yake kwa weledi,
2: Tasnia ya habari isiwe
hatarini, waandishi wa habari wakiuawa na Watu wasiadhibiwe kila mtu atogopa
kuwa mwanahabari
3: Wasijulikane, kwani kunaweza
kuwaweka katika hatari.
Hata hivyo, amesema ili kuzuia
majanga hatari yanayowakumba waandishi, ni pamoja na kuwepo kwa mifumo ya kudai
haki za binadamu kuanzia ngazi ya Kimataifa na Kikanda ili haki za waandishi wa
habari ziweze kupatikana.
0 Comments