📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
HAYO yamebainishwa jijini Dodoma mwishoni mwa Juma lilopita na Mchungaji wa kanisa la Waadventista Wasabato mtaa wa chuo Kikuu cha Dodoma,Mch. Bunga Edward Dettu katika makabidhiano ya uongozi Mpya wa chama cha Wanafunzi Waadventista Wasabato Vyuo vya kati na vyuo vikuu(TUCASA)kanda ya chuo Kikuu cha Dodoma .
Mch.Bunga amesema Viongozi ni wajibu muhimu kuonesha njia na malengo na mipango kwa maendeleo ya kanisa .
“Vijana wa TUCASA ni nyenzo muhimu sana katika kufanikisha masuala ya utume hivyo katika tukio hili muhimu la kukabidhiana madaraka nimewaasa viongozi wa TUCASA wapya kuonesha njia pamoja na kukabiliana na changamoto katika maeneo ya vyuo maana changamoto zozote ni za kuja na kuzitatua ,hakuna changamoto zinazodumu milele”amesema
Aidha,Mch.Bunga aliwahimiza wanachama wa TUCASA kuendelea kuwa wa mfano wa kuigwa kwa watu wengine katika kuonesha njia iliyo bora na impendezayo Mungu kwa kufanya matendo mema .
Mkurugenzi idara ya champlasia na huduma za vijana kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kati mwa Tanzania(CTF) Mch. Sabato Maseke alihimiza Wanatucasa kuongeza kasi ya utume katika maeneo ya vyuo.
“Mungu ametupatia fursa ya pekee ya kuwa na wanafunzi wenzetu wasiomjua Mungu katika maeneo ya vyuo,kwa hiyo niwaase wanafunzi wa UDOM na Tanzania kwa ujumla kutumia nafasi walizonazo vyuoni kuwahubiria habari njema za neno la Mungu wanafunzi wengine walio karibu nao”amesema.
Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo wa Champlasia na huduma za vijana kanisa la Waadventista Wasabato jimbo la kati mwa Tanzania[CTF] alisema tukio la makabidhiano ya Uongozi TUCASA chuo Kikuu cha Dodoma limekwenda sambamba na utunukiwaji wa vyeti kwa viongozi wakuu chama cha vijana kanisani[Master Guard] waliosoma kozi ya Msingi huku akiwaasa vijana kujiunga na chama cha vijana kanisani.
Nao baadhi ya viongozi wastaafu wa TUCASA waliokabidhi madaraka kwa viongozi wapya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM ) akiwemo kiongozi wa mstaafu idara ya Mawasiliano Yohana Zabron amesema ushirikiano ndio nyenzo Naye Mwenyekiti Mstaafu Daniel Tumaini ametoa wito kwa viongozi wapya kumtegemea Mungu katika kufanikisha kazi za Utume pia akibainisha kuwa yupo tayari kutoa ushauri.
Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa TUCASA UDOM kwa mwaka 2021/2022 Yusufu Jonas Kitululu alisema atakuwa pamoja na wana TUCASA wote katika kuifanya kazi ya utume na yupo tayari kupokea ushauri kwa maendeleo ya utume chuoni. .
Miongoni mwa majukumu
ya viongozi wa Chama cha Wanafunzi wa kiadventista Wasabato vyuo vya kati na
vyuo vikuu ni kuhakikisha wanaeneza uinjilisti maeneo ya chuo.
0 Comments