📌JOSEPHINE MAJURA(WFM)
WIZARA ya Fedha na Mipango imepokea na kuanza kuyafanyia kazi maagizo ya
Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuhusu misamaha ya kodi kwa fedha za
misaada ili kutekeleza miradi ya vipaumbele.
Hayo yameelezwa jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi wa
Balozi wa Japan nchini, Niinuma Takashi, ambaye alilalamikia suala la kodi kwa
fedha za mikopo na misaada inayotolewa na nchi hiyo.
Dkt. Nchemba alieleza kuwa Mhe. Rais ametoa maagizo hayo kwasababu fedha
za msaada zikitolewa kwa ajili ya kusaidia jamii na hata zikitozwa kodi pia
kodi hiyo itatumika kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya nchi na wananchi kwa
ujumla.
Hili jambo tunalifanyia kazi na mpaka sasa tumeshaandaa waraka na tunasubiri ratiba ya Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuupitisha katika baraza hilo ili ukidhi matakwa ya kisheria.
Dkt. Nchemba.
Alimuhakikishia Mwakilishi wa Balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania
itaendelea kushirikiana na Japan katika nyanja mbalimbali kwa maendeleo ya nchi
zote mbili.
Aliongeza kuwa endapo changamoto ya misamaha ya kodi itaondolewa kwenye
fedha za misaada na mikopo inayotolewa, uhusiano wa Tanzania na wadau wa
maendeleo utazidi kuimarika na kubainisha kuwa nchi yake ipo tayari kupokea
maombi mapya ya kufadhili miradi mipya ya kipaumbele.
Ujumbe kutoka
Tanzania ukiongozwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck
Nchemba (Mb) (wa tano kulia) wakimsikiliza Mwakilishi wa Balozi wa Japan nchini
Bw. Niinuma Takashi (kushoto)
0 Comments