📌ANGELA MSIMBIRA- TAMISEMI
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy
Mwalimu amewaagiza watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanajenga mahusiano mazuri na
baraza la madiwani ili kuweza kutimiza
malengo ya serikali ya kufikisha huduma bora kwa wananchi.
Waziri
Ummy ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na Menejimenti ya Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino, Jijini Dodoma mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo
inayotekelezwa na Halmashauri hiyo
Amewataka
wataalam kuhakikisha wanazingatia
ushauri wa baraza la
madiwani kwa kuchuja masuala ya
muhimu na yanayoonekana yanaenda kinyume
na sheria na taratibu wawashirikishe Wakuu wa Mikoa.
Msiwadharau Madiwani na kudhani hawajasoma, wapo madiwani wana elimu ya kutosha,hao ndio wawakilishi wa wananchi na wamechaguliwa na wananchi wapeni ushirikiano ili kuleta maendeleo katika Halmashauri zetu
Waziri Ummy
Amefafanua
kuwa madiwani ndio wawakilishi wa wananchi na wamechaguliwa kwa ajili ya
kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili , hivyo ni vyema
watendaji wa Halmashauri wakahakikisha wanaimarisha mahusiano katika utendaji
kazi na baraza la madiwani ili kuleta
mabadiliko na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika Halmashauri.
Wakati
huohuo Waziri Ummy amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya chamwino
Athumani Masasi kujenga mahusiano mazuri na watumishi wa Halmashauri hiyo ili
kuhakikisha wanaweka mikakati ya ukusanyaji wa mapato kutokana na halmashauri
hiyo kutokufanya vizuri katika ukusanyaji wa Mapato.
Aidha
amemuagiza Mweka hazina wa Halmashauri hiyokuhakikisha anapeleka benki kiasi
cha shilingi milioni 139 hadi kufikia tarehe 15/04/20201 fedha ambazo
zilikusanywa lakini hazikuwekwa benki
0 Comments