📌WAMJW-DODOMA
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka watumishi wa Wizara hiyo pamoja na Sekta ya Afya kwa ujumla kukubali mabadiliko ya uongozi na kuangalia namna ya uendeshaji ili kuzidisha uweledi katika maeneo yao ya kazi.
Waziri Gwajima amesema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwapokea viongozi wapya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuapishwa mapema wiki hii.
Viongozi hao ni Katibu Mkuu Prof. Abel Makubi pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale ambao leo wameripoti rasmi ofisi za Wizara jijini Dodoma.
Tuimalishe mifumo ya kufanya kazi pamoja kama tulivyoimarisha mifumo ya kufanya na mataifa mengine, tuna makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kutekeleza dira ya afya duniani. Tunashindwaje kuwa na makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika kutekeleza sera yetu?
Waziri Gwajima ameongeza kuwa kuna watu huwa wanaanzisha ajenda ambazo kimsingi Wizara inakua haina haja nazo huku akitoa onyo kwa watumishi wa Wizara ya Afya pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoandaa vikao ambavyo ajenda zake zinakua siyo za kueleweka.
Aidha, Waziri Gwajima ameagiza wakurugenzi wa idara
zilizopo Wizarani kutengeneza vikao vya mashirikiano ili kuwezesha mnyororo wa
kutoa huduma za afya kufanyika kwa uweledi na kuepusha malalamiko kutoka kwa
wananchi.
0 Comments