📌MWANDISHI WETU
WIZARA ya Maliasili na Utalii imefunga rasmi mzozo uliodumu kwa miaka miwili juu ya eneo la uwindaji kando ya ziwa Natron ambalo lilihusisha Wizara, wilaya ya Longido na kampuni za uwindaji zinazofanya kazi katika eneo hilo, ambao ulionekana kudhoofisha sekta ya uwindanji na utalii kwa muda mrefu.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa kusoma hukumu ya Maombi ya Marejeo(Admistrative Review) iliyowasilishwa na kampuni ya Green Miles Safari Limited (GSML) walimwomba Waziri afutilie mbali uamuzi ambao ulipitishwa na ofisi yake wa kufuta leseni ya kitalu cha uwindaji cha Ziwa Natron Mashariki kinachomilikiwa na kampuni hiyo.
Dk Ndumbaro amesema kuwa baada ya kupitia na kuzingatia kwa ushahidi wa pande zote zinazokinzana kwenye mgogoro
huo, ameamua kutengua uamuzi na kuongeza kuwa uamuzi huo ulikuwa batili hivyo
GSML watakuwa na haki ya kuendesha shughuli zao katika kitalu hicho.
Mzozo huo
ulishika kasi mnamo Agosti 7,2019,Waziri wa Maliasili na Utalii wa wakati huo Dk Hamis Kigwangala aliandika
barua kwa kampuni hiyo kuwataka kusitisha shughuli zao katika kitalu hicho, Dkt
Ndumbaro amesema barua hiyo ilikuwa ni kinyume na matakwa ya Sheria
ya Uhifadhi wa Wanyamapori Namba 5 ya 2019 kwa vile haikuonesha kosa la kampuni hiyo.
Barua kutoka kwa Waziri Dkt.Kigwangala kwenda GMSL, (kumb CBA.177 / 389/01/281) ya tarehe 7 Agosti 2019 haikuonyesha sababu yoyote ya kuhalalisha uamuzi wake wa kufuta umiliki wa kitalu hicho, uamuzi huo unapingana na kifungu cha 38 (12) cha sheria hiyo
Dkt. Ndumbaro
Sehemu hiyo ya sheria inaelekeza kwamba Waziri anaweza, wakati wowote kabla ya kumalizika kwa kipindi cha uwindaji, kufuta leseni ya kitalu cha uwindaji ikiwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba mmiliki ameshindwa kulipa kodi au kutoa taarifa za uongo wakati wa mchakato wa ugawaji wa kitalu hicho.
Sehemu
hiyo pia inatoa mwongozo kwa waziri anapaswa kufuta leseni ikiwa mmiliki wa
leseni amehukumiwa kwa moja ya kosa lililopo
chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, ameshindwa kulipa ada
zinazohitajika au deni lingine lolote na eneo lake la uwindaji.
Mbele yangu sina Ushahidi unaonesha kuwa kabla ya kufutiwa umilikiwa kitalu cha uwindaji Muomba Mapitio (GSML) alijulishwa kosa lake na kupewa sababu za uamuzi kama ambavyo kifungu cha sheria kinataka.
Dkt.Ndumbaro.
Walakini,
Dk Ndumbaro amesema mbali ya sababu iliyotajwa hapo juu, uamuzi wa Waziri wa
wakati huo pia haujatoa fursa kwa GSML kusikilizwa kabla ya kufukuzwa
katika kitalu hicho
, Dkt.Ndumbaro amesema hiyo inapingana
na kanuni ya haki ya asili (Nature Justice) kama inavyoonyeshwa katika Sheria
ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sehemu 38 (13).
Uamuzi wa kubatilisha umiliki wa GMSL katika kitalu hicho haukufuata mahitaji ya kisheria na kanuni za utawala bora.
Dkt. Ndumbaro.
Mkurugenzi wa Green Miles Safari Awadh Abdallah akitoa ushahidi wake katika kikao kilichofanyika mwezi Machi jijini Dodoma |
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa GSML, mshauri wa kampuni hiyo Salim Balleith alitoa shukrani zake za dhati kwa Serikali kwa uamuzi huo ambao unawapa haki ya kufanya kazi katika kuzuia hadi 2022.
GSML imesema haitochukua
hatua zaidi kama vile kudai fidia kutokana na uharibifu wa mali katika kambi zao za uwindaji ndani ya eneo hilo
GSML haitachukua hatua zaidi dhidi ya Wizara kwa kile kilichotokea. Sisi ni watanzania wazalendo, tulichotaka ni haki yetu tu ya kufanya biashara hiyo katika eneo hilo.
Salim Balieth
0 Comments