📌HAMIDA RAMADHANI
WAZIRI wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amewataka wataalamu wa zao la Pamba kuwasaidia wakulima waweze kulima Kilimo chenye tija katika zao hilo.
Akizungumza leo jijini hapa katika kikao cha awali cha Bodi ya Pamba amesema Wizara hiyo ipo mbioni kuanzisha Mfuko wa Utafiti ambao utawasaidia wakulima kulima Kilimo chenye tija.
Amesema zao la Pamba, limekua na changamoto ya kupanda na kushuka ambapo tatizo kubwa limeonekana ni ukosefu wa pembejeo huduma za ugani hali ya hewa,na utulivu wa Soko.
Pembejeo na huduma za ugani zimekua zikiendeshwa kwa sera,ambazo tumezitunga Sisi,sasa ni lazima tuweke sera nzuri ambazo zitamsaidia mkulima kulima kilimo chenye tija
Profesa Mkenda
Amesema Pamba ni zao muhimu kiuchumi na kisiasa na limekua likigusa Watu wengi nchini hivyo hatuna budi kuwekea mkazo ili wakulima waweze kulima mazao yenye tija.
Aidha amesema kwa mwaka 2021 Tanzania inatarajia kupata tani takribani laki nne ambapo ni tofauti na miaka ya nyuma.
Mwaka huu wa Kilimo ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo tunatarajia kupata tani laki 393,460 kwa miaka kumi hatujawahi kufikia tutakuwa na msimu mzuri
Mkenda
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga ameiomba serikali kutengeneza mfumo utakaoweza kuwapatia maafisa ugani pikipiki na kujaziwa Mafuta ili maafisa ugani waweze kupita kwenye mashamba ya wakulima kukagua na kubaini athari mapema za wadudu wekundu.
"Tunaomba hata hizi pikipiki za maafisa ugani zifungwe GPS ili afisa ugani aweze kutambulika anafanyia shughuli gani,na ni kwa wakati gani " amesema Mtunga
Hata hivyo ameiomba serikali
kumaliza deni la Shilingi billion 87,na ambapo amesema endapo madeni hayo
yatatatuliwa zao la pamba litasonga mbele.
0 Comments