📌FAUSTINE GIMU GALAFONI.
KATIKA kuhakikisha sekta ya kilimo inaendelea kukua hapa
nchini,zaidi ya wakulima elfu 50 kutoka kata 3 Mkoani Dodoma
wamenufaika na mafunzo ya mradi wa kilimo cha mazao yanayohimili
ukame ikiwemo mtama,uwele na ulezi chini ya chini ya Taasisi ya Utafiti wa
kilimo nchini[TARI]kituo cha Hombolo.
Akizungumza katika siku maalum iliyotengwa kwa ajili ya kutoa
mafunzo hayo mahsusi kwa wakulima ,mratibu idara ya utafiti na ubunifu kituo
cha utafiti wa kilimo[TARI] Hombolo Dkt.Eliud Kongola amesema
wanatoa huduma za utafiti kwa mazao yanayovumilia ukame hususan Mtama,Uwele na
Ulezi ambapo ni zaidi ya wakulima elfu 50 wanapata huduma za ugani kwa
kata tatu za Hombolo Bwawani,Hombolo Makulu pamoja na Ipala katika jiji
la Dodoma.
“Kituo chetu kinahudumia wakulima wanaolima yanayovumilia ukame
ikiwemo ,uwele,mtama na ulezi hivyo tumekuwa tukishirikiana halmashauri
ya jiji la Dodoma tuna zaidi ya wakulima 50,000 wananufaika na mashamba
darasa haya hususan kutoka kata 3 zinazozunguka kituo cha utafiti wa
kilimo[TARI]Hombolo”amesema.
Mratibu wa uaushaji wa Teknolojia
kituo cha utafiti wa kilimo [TARI] Hombolo Erinesa Sanga amesema
shamba darasa linamfanya mkulima aelewe zaidi huku Diwani wa Hombolo
Makulu Kamishna Gidion Kana akiipongeza TARI kwa utafiti huo kwa vitendo.
Nao baadhi ya Wakulima wameelezea jinsi walivyonufaika na
mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kuvuna mazao maradufu
zaidi ikilinganishwa na hapo awali.
“Mwanzoni nilikuwa navuna magunia matatu kwa hekta moja lakini
baada ya kujifunza kilimo hiki cha kisasa kupitia mashamba darasa nimeanza
kuvuna kiasi cha magunia kuanzia 10 na zaidi ,imekuwa faraja kubwa”amesema mmoja wa wakulima.
0 Comments