📌ALEX SONNA
VIJANA 48,000 katika Mikoa Minne wanatarajia
kupata elimu ya utunzaji wa mazingira na usafi wa Mwili kupitia shirika Lisilo
la Kiserikali la Raleigh Tanzania wanaoendesha mradi wa “Vijana na mabadiliko
chanya kitabia juu ya usafi” ili kubadilisha tabia na kuepuka Magonjwa
Mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa mradi huo
Augustino Dickson, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
vijana walio katika maradi huo kufanya usafi katika soko la Mavunde Chang’ombe
pamoja na kutoa semina kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma.
Bw.Dickson amesema kuwa mradi huo hivi sasa
unatekelezwa katika mikoa ya Dar es saalam, Dodoma, Morogoro pamoja na Iringa.
Amesema kuwa mradi huo umelenga katika kubadilisha
mitazamo ya vijana katika masuala ya usafi ambayo yamekuwa hayapewi kipaumbele
hali inayosababisha uchafu kuzagaa katika maeneo mengi.
Mradi wetu umelenga kuleta mabadiliko chanya kitabia kwa vijana na unahusisha vijana kutoa mafunzo kwa vijana wenzao ili kupanua wigo wa uelewa juu ya usafi na mazingira
Dickson.
Aidha amesema kuwa kupitia mradi huo walifanya tafiti kuona ni jinsi gani wanaweza kuendesha mafunzo ya usafi kwa vijana ili kuwabadili mitazamo yao.
“Vijana ndiyo kundi kubwa katika taifa hivyo tuliona kuwa kwa kuwataumia wao tutaweza kubadili mitazamo iliyopo katika jamii na kuleta mabadiliko chanya katika suala la usafi”amesisitiza
Hata hivyo amesema kuwa pamoja na kutoa mafunzo haya lakini pia wamekuwa wakishirikiana katika kufanya usafi katika maeneo mbalimbali na kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia uasafi na kuhifadhia taka katika maeneo kama walivyofanya ambavyo leo katika soko la Mavunde Chang’ombe na shule ya sekondari ya Dodoma.
Kwa upande wake Afisa afya jiji la Dodoma Abdallah Mahia amesema, kutoa elimu katika shule kutasaidia wa wanafunzi kukua katika mazingira ya kutambua umuhimu wa usafi ili kupepukana na magonjwa ya mlipuko.
Sisi kama serikali Kwa kushirikiana na Wizaraya Afya na Tamisemi, tunaungana nanyi katika kuhamasisha uelewa wa kufanya usafi na kutunza mazingira.
Mahia.
Naye Mmoja wa vijana wanufaika wa mafunzo hayo Dorice Kimambo, amesema kuwa wamejifunza mambo mbalimbali yanayohusu usafi na baadaye wanaenda katika jamii kutoa elimu na kusaidia kubadili mitazamo iliyopo juu ya usafi.
“Katika maeneo tunayokwenda kutoa elimu tumebaini bado zipo changamoto kadhaa ikiwemo watu kuishi kwa mazoea imekuwa kikwazo kupata mabadiliko kwa haraka, watu wengi wanadai kuwa hawana fedha za kununulia vifaa vya kuhifadhia taka au kulipia magari ya kubeba taka”amesema Kimambo
Shirika la Raleigh Tanzania limeendesha Zoezi la Usafi Katika Soko la Mavunde la Chang’ombe pamoja na kutoa elimu katika Shule ya Sekondari Dodoma ikiwa ni katika kuadhimisha kilele cha mradi huo ulioratibiwa miezi miwili iliyopita.
0 Comments