📌DEVOTHA SONGORWA.
JUMUIA ya Wanawake Tanzania ( UWT)
imeahidi kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa majukumu
yake kwa ajili ya manufaa ya watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari
ili kutoa tamko la Jumuia,Mwenyekiti wa UWT Taifa,Gaudensia Kabaka
alisema Chama kinamuamini kwani aliyoonyesha uwezo wake wa uongozi akiwa
nafasi ya Makamu wa Rais.
Amesema UWT inampongeza kwa
kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania mwanamke licha ya kupata nafasi hiyo
katika hali ya majonzi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk.
John Magufuli.
Amesema anaamini nchi iko salama
chini ya uongozi wake kwani amekuwa na uwezo mkubwa wa kiutawala na uongozi hata
wakati akiwa nafasi ya Makamu wa Rais hivyo watanzania wamuamini na kumpa
ushirikiano wa kutosha ili nchi iweze kusonga mbele.
"Tulipokea kwa masikitiko na
simamzi kubwa taarifa za kifo cha Rais wetu hatujawahi kupata msiba wa kiongozi
mkubwa hivyo akiwa madarakani tunatoa pole kwa watanzania wote,"alisema.
Pia Mwenyekiti huyo alieleza kwamba
UWT inaungana Serikali KWA ujumla chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika
muendelezo wa siku 21 za maombolezo huku ikitoa pole kwa Rais Samia kwa msiba
huo mkubwa kwa Taifa.
"Tunaendelea kuwa pamoja naye
tunapoendelea katika siku 21 za maombolezo ya msiba huu mzito kwetu na
tunampongeza kwa utulivu aliuonyesha wakati wote wa msiba maana sisi watanzania
tulikuwa tunamwangalia yeye lakini alikuwa mtulivu Sana hali iliyotufanya nasi
watanzania kuungana pamoja," alieleza Gaudensia.
Hata hivyo amempongeza Rais Samia
Suluhu Hassan kwa kuwa mwanachama hai ndani ya Chama hatua iliyoonyesha mfano
huku UWT ikijipngeza kwa kutoa Rais mwanamke hatari inayotoa chachu kwa kina
mama kuthubutu kushika nafasi za uongozi.
Akizungumzia mwenendo wa utendaji
wake akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alieleza kwamba ameanza
vizuri kwa kumteua Dk.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais pamoja na viongozi
wengine wakiwemo Mawaziri na Manaibu Waziri.
" Sisi kina mama na watanzania
wote tunakubaliana naye kuwa Makamu wa Rais anaendelea akamteua Balozi Hussein
Othuman kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kwakweli ameanza vizuri tunaamini watafanya
Kazi vizuri kuwatumikia wananchi," alibainisha.
Kuhusu upande wa Afrika Mashariki
alibainisha kwamba Tanzania ilikuwa nchi ya pili kuwa na Makamu wa Rais
mwanamke ikifuatia nchi ya Uganda lakini kulingana na Katiba ya Tanzania mama
Samia Suluhu Hassani anakuwa Rais kamili ikilinganisha na Katiba za baadhi ya
nchi zingine ambavyo angekaimu nafasi hiyo kwa muda.
"Kwa kweli Rais Samia ana sifa
zote za kuwa Rais licha ya taratibu za Katiba kwamba Rais akifariki Makamu
ndiye anachukua nafasi bado ana sifa za kuwa Rais na kufuatia uongozi wake kama
Makamu alimsaidia Hayati Rais.Dk.Magufuli,"alieleza.
Aidha alifafanua kwamba uamuzi wa
kutoa nafasi kubwa za uongozi kwa wanawake katika Baraza la Mawaziri
umeongeza idadi yao hali inayoendelea kutoa hamasa kwa wanawake kujituma na
kuonyesha uwezo wao.
"Zipo Wizara ambazo tunaamini
zinawagusa wananchi moja zaidi ipo Wizara ya Afya, Wizara ya elimu,Wizara ya
mambo ya nje,Wizara ya TAMISEMI , Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Watu
wenye ulemavu na Wizara ya Maji tuna Naibu Waziri mwanamke anaamini watachapa
Kazi,"alisema.
Alihitimisha kwa kuwasihi viongozi
wote walioteuliwa au kuendelea na nafasi zao kuviishi viapo vyao kwa
kuwatumikia wananchi na kutokuwa wabadhirifu wa mali za umma,kulinda Katiba na
kutekeleza miradi iliyoanishwa kwa mujibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
pmaoaja na watanzania wote kukupa kodi kwa Maendeleo ya Taifa kama sehemu ya
kumuenzi Hayati Rais Dk. John Magufuli.
0 Comments