📌FAUSTINE
GIMU GALAFONI
HAYO yamebainishwa
leo April 29,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri
mkuu,Sera,Uratibu,Bunge ,Kazi ,Ajira , vijana Patrobas Katambi katika ufunguzi
wa mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza miradi ya wasichana balehe na
wanawake vijana .
Naibu waziri
Katambi amesema utafiti wa mwaka 2016/17 umeonesha kuwa
kiwango cha ushamiri kimeendelea kupungua sambamba na kiwango cha maambukizi
mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI, Wastani wa Kitaifa ushamiri wa VVU ni wa
asilimia 4.7,Mikoa yenye ushamiri wa juu ni Njombe (11.4%) na Iringa 11.3 na
Mbeya (9.3%) ambapo ushamiri katika Mkoa wa Dodoma umeongezeka kutoka asilimia
2.9 hadi asilimia 5.
Mhe.Katambi amefafanua kuwa Katika utafiti huo watu 72,000 wanapata maambukizi mapya kwa mwaka na kati yao 40% ni vijana; kati ya hao vijana 80% ni wasichana wa umri wa miaka 15 – 24 ikimaanisha kuwa kila kundi la vijana kumi wenye maambukizi 8 kati yao ni vijana wa kike na 2 ni vijana wa kiume.
Ni muhimu kuhimiza vijana na watu wote kupima ili kujua hali zao, kutumia dawa kwa waliogundulika na VVU na kuepuka maambukizi ikiwa bado hawajapata maambukizi.
Katambi
Aidha,
Katambi amesema kupitia matokeo ya utafiti wa 2016/17 Serikali iliona
umuhimu wa kufanya jitahada za pamoja na wadau katika mapambano dhidi ya VVU na
UKIMWI, hususan katika kundi la vijana wa kike.
Katambi amesema malengo ya nchi ni kufikia sifuri ya maambukizi mapya ya VVU, sifuri ya ubaguzi na unyanyapaa utokaonao na UKIMWI na sifuri ya vifo vitokanavyo na UKIMWI ifikapo 2030.
Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu Tume
ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS),Dk.Leonard Maboko amesema kuwa lengo la
kikao hicho ni kuwaleta wadau na kuona wamefikia wapi na wamekutana na
changamoto zipi pamoja na kuzitatua.
"Sisi TACAIDS kazi yetu ni
kuratibu na ndio maana hapa kuna taasisi kazi yetu kubwa ya hili kundi ni
kuratibu kila mwaka hivyo hichi kikao ni cha kuwaleta hawa wadau kuona
wamefikia wapi na wamekutana na changamoto zipi pamoja na kuzitatua,ili
kujadiliana tulipotoka tulipo na tunapoelekea,"amesema Maboko.
Dkt.Maboko amesema kuwa Waziri
Mkuu,Kassim Majaliwa aliagiza Tacaids ifanye kazi na vijana ambapo alidai kwa
sasa wanafanya kazi nao hususan wasanii.
Hata hivyo Dkt.Maboko amesema kuwa
takwimu zinaonesha vijana ni kundi lenye Changamoto katika maambukizi ya
Ukimwi.
"Maambukizi mapya asilimia 40
yalikuwa yanatokea kwa vijana lakini asilimia 80 ya hao vijana ni wa kike,kwa
umaalumu kabisa ndio maana hili kundi likapewa msisitizo huu.Takwimu
zilituonesha hivyo tukaona kuna haja ya kuweka mkazo katika hili,"amesema
UMEISOMA HII?👇👇👇
0 Comments