TANZANIA NA MAREKANI KUKUZA SEKTA YA VIWANDA NA UWEKEZAJI

 


📌DEVOTHA SONGORWA

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   imesema itaweka mpango rafiki wa  kuhakikisha inakuza sekta ya biashara na uwekezaji kati yake na nchi ya Marekani.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof.Kitila Mkumbo katika kikao kazi kilichokutanisha Wizara ya Uwekezaji,Wizara ya Viwanda na Biashara na Balozi wa Marekani nchini Tanzania kwa lengo la kujadili namna ya kuboresha sekta hizo katika kukuza uchumi wa nchi zote mbili na raia wake.

Prof.Mkumbo alisema kwamba kilichojadiliwa ni namna ya kutunza biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Marekani na kuboresha mpango uliopo wa biashara ambao tayari umewezesha baadhi ya bidhaa za Tanzania kufanikiwa kuuzwa nchini Marekani.

Tumeangalia fursa ambazo zipo na sisi kama Tanznia tumeona tuna fursa bado wafanyabiashara wetu hawajatumia fursa hii ya kupeleka  bidhaa kule na sisi tutafanya kila liwezekanalo kuwawezesha wafanyabiashara wetu kuuza bidhaa zao Marekani tuongeze wigo wa mapato yetu.

Prof. Mkumbo.

Akizungumzia suala la uchakataji wa mazao alisema kwamba ni nia ya serikali kuweka mazingira rafiki ya uchakataji wa mazo kutoa mwanya wa kuuzika nchini Marekani kwa kupelekwa kama malighafi.

“Mazao yatokanayo na kilimo ni nia yetu kuwezesha uchakataji hapa nyumbani ili tusafirishe bidhaa amabzo zimeshasindikwa ziwe zimekamilika kama matunda,korosho, mananasi mazungumzo yamekuwa mazuri sana tunatarajia mafanikio makubwa kati yetu kwa manufaa ya wananchi wetu,”alieleza Waziri huyo.

Aidha kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili alibainisha kwamba wamekubaliana kuendelea kulinda uhusiano wa nchi hizo uliodumu kwa muda mrefu uliojengwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano,Hayati Dk.John Magufuli.

Tuko tayari kuendeleza mashirikiano baina yetu na Marekani yaliyokuwepo tangu utawala wa Aliyekuwa Rais Hayati,Dk.John Magufuli hadi sasa ni Rais Samia Suluhu Hassani na mwaka huu tunaadhimisha miaka 60 ya mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Marekani yazidi kukua

Kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji,Geofrey Mwambe alisema  kuwa baadhi ya makubaliano ni pamoja na kuwa na mijadala ya mara kwa mara kati yao na wawekezaji kutoka marekani, Marekani kuwa na utayari wa kuwekeza nchini huku akisema kwamba hatua ya Rais Samia kutenga kuwa Wizara inayojitegemea ni ishara ya namna serikali inavyodhamiria kuinua Nyanja ya uwekezaji .

“Tunawahakikishia kujenga mazingira wezeshi ya uwekezaji na tulitamani kufanya Investment forum nyingi Marekani tukiach aprofram ya hapa ya kuwasikiliza kwamba wana changamoto gani pia hata kuwaendea na kuwaomn akufanya ufahamu wa  fursa zilizopo kwetu  kama sehemu ya kufikia dira ya maendeleo ya mwaka 2025 na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),alieleza Mwambe.

Naye Balozi wa Marekani nchini Tanzani,Don Wright alisema uimarishwaji wa uhusiano katika ya Marekani na Tanznia kupiyia sekta ya Viwanda na Biashara utasaidia vijana kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na changamoto ya ajira huku akiahidi kuipatia Tanzania ushirikiano kufikia malengo yaliyokususdiwa.

Post a Comment

0 Comments