TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma inamshikilia Luka Nkini mwenye umri wa miaka 38,mkazi wa Airport jijini Dodoma kwa tuhuma za kujifanya mganga wa kienyeji huku akiwataka baadhi ya wakina mama kingono kama sharti la kuwasaidia ambapo amejipatia kiasi cha Sh.Milioni 105 na viwanja viwili.
Hayo yameelezwa leo Jijini Dodoma na Mkuu wa
TAKUKURU Mkoa wa Dodoma,Sostheness
Kibwengo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu utendaji wao wa
kazi kwa robo ya Januari hadi mwezi Machi Mwaka huu.
Kibwengo amebainisha kuwa mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na Sheria ya
kuzuia na kupambana na rushwa sura namba 329 marejeo ya mwaka 2019.
Aidha amewataja wahalifu wengine ambao walikuwa
wakishirikiana na Mtuhumiwa Nkini kuwa ni
Hussein Mvungi(44)mkazi wa Himo Mkoani Kilimanjaro ambaye nae
ameshakamatwa na amekiri tuhuma dhidi yake pamoja na Bw. John Gabriel Munuo
mkazi wa Sanyajuu Siha huku akimtaka Bwana Munuo kuripoti mara moja kwenye Ofisi za Takukuru ambazo zipo karibu naye
kabla ya rungu la Takukuru halijamfikia.
Katika hatua nyingine Kibwengo amesema kuwa wameweza kuokoa zaidi ya Shilingi milioni900
pamoja na Nyumba moja na kiwanja kimoja
ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha sh Milioni 214,182,548 ni fedha ambazo
zilikuwa haziwasilishwi NSSF na waajiri.
ANGALIA ZAIDI KWENYE CPC TV👇👇👇
0 Comments