📌MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge
ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Dodoma (DUWASA)
kukabiliana na wezi wa maji huku wakiwachukulia hatua watumishi wa mamlaka hiyo wanaochangia hasara kwa kutokuwa waaminifu.
Akizungumza mapema leo katika semina ya wenyeviti na
watendaji wa mitaa Jijini Dodoma Dkt.Mahenge amesama kuwa baadhi ya watumishi
wa Mamlaka hiyo sio waaminifu na wanaingiza hasara ya mapato kwa kushirikiana
na wananchi hivyo ni vyema wakawachukulia hatua ili kudhibiti wezi wa maji.
Tuhakikishe kuwa tunakabiliana na wezi wa maji na waharibifu wa miundombinu,wale wanaoiba vizibo na mifunuko ya maji taka kwa kuwa sheria zipo wakamatwe na wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni zake,simamieni na wale ambao siyo waminifu wanao ''kula dili'' na wananchi za kuhusu kutumia maji bila malipo wakamatwe waondolewe kwenye utumishi wa DUWASA maana hao hawafai
RC Mahenge.
Katika hatua nyingine Dkt Mahenge ameipongeza
Duwasa kwa jitihada kubwa inayofanya kuhakikisha inakabiliana na changamoto ya
upatikanaji wa maji kwani hadi sasa jiji la Dodoma linaupugufu wa maji zaidi ya
lita million 37 kufuatia kuzalisha lita Milion 103.
“Niwapongeze sana DUWASA kwa kuzalisha lita million
66 wakati kabla Serikali haijamia Dodoma tulikuwa tunazalisha lita million 61.5
kwa hiyo lipo ongezeko kubwa,niwapongeze kwa kuongeza uzalishaji wa maji na
maji tunayozalisha sasa lazma tuyatunze na tuyalinde” Aliongeza RC Mahenge.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti
wa bodi ya DUWASA,Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Neema Majule amesema
maji ni kapaumbele na DUWASA imefanya kazi kubwa kukidhi mahitaji ya maji
kutokana na ongezeko la watu Dodoma.
Duwasa imefanya kazi kubwa sana kipindi hiki ili kuweza kukidhi mahitaji ya maji na kukidhi ongezeko la watu Dodoma,Mtakubaliana na mimi kwa sasa kuna unafuu mkubwa sana hata kama kuna upungufu wa maji na hata kama kuna mgao wa maji lakini kwa kiasi kikubwa sana maji yameweza kutosheleza kwa jiji la Dodoma
Majule.
Naye Mbunge wa Dodoma Mjini Mh Antony Mavunde
amebainisha kuwa Kuanzia mwezi wa kumi na moja hadi sasa visima 10 vya maji
vimechimbwa kati ya visima 20.
“Na mimi kama mbunge kwenye jimbo hili naunga mkono
jitihada za DUWASA kwenye kutatua changamoto hasa katika maeneo yaliyo
pembezoni mpaka hivi sasa toka mwezi wa kumi na moja mwaka jana tumeshachimba
visima kumi kati ya visima 20 nilivyoviahidi wakati wa kampeni na ninaamini
vingine tutavikamilisha kwa wakati” Amesema Mavunde.
Aidha kukamilika kwa miradi miwili ya maji jijini
Dodoma Mradi wa Farkwa na ule wa Ziwa Victoria inatajwa kuwa itasaidia kwa
kiasikikubwa kuondoa adha ya upatikanaji wa maji kwa wananchi.
0 Comments