📌HAMIDA RAMADHANI
MSEMAJI Mkuu wa
Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa
amewataka waandishi wa habari hapa nchini kuzingatia Sheria ,Kanuni,taratibu
,Miongozo na Taaluma ya uandishi wa habari Katika utekelezaji wa majukumu yao.
Msigwa ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma mara baada ya
kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa
Idara hiyo Dkt Hassan Abasi aliyehudumu katika nafasi hiyo katika kipindi cha
miaka minne na miezi minane.
Wakati huo huo amesema atasikitika kuona kuwa Waandishi wa Habari na Vyombo vya habari vinatumika kwaajili ya kuibomoa nchi,serikali na kurudisha nyuma juhudi zilizofanywa na watanzania tangu Tanzania ipate uhuru.
Katika hatua nyingine Msigwa amesema haikubaliki
kwa mwandishi wa habari kunyanyaswa kwa namna yeyote ile pindi anapokwenda
kutekeleza majukumu yake ya kazi.
Kwa upande wa aliyekuwa Msemaji Mkuu wa serikali Dkt Abas
ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo
amemshukuru Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwa nafasi aliyo mpa wakati ule na
kumshukuru Rais Samiah Suluhu Hasan kwa kuendelea kumuamini katika kuitumikia
nchi.
Leo Ndugu Msigwa nakukabidhi majukumu haya sisemi ulikotoka ulikuwa unalala, hapana. Ila kazi hii ya Usemaji haulali katika saa 24 na hata ukilala inabidi ulale kimkakati.
Dkt Abbasi
Dkt. Abbasi alimpongeza Bw. Msigwa kwa uteuzi huo na kueleza kuwa anaamini atafanikiwa kuendeleza pale yeye alipoishia.
0 Comments