📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
MKUTANO wa saba wa Mawaziri wa nchi
za Afrika zinazozalisha madini ya Almasi umefanyika leo
huku ukitaraijiwa kuhitimishwa kesho kwa njia ya video ambao
utahusisha ushiriki wa Mawaziri wa nchi wanachama na wataalamu wa madini kutoka
nchi 12.
Hayo yamebainishwa leo
Jijini Dodoma na Waziri wa Madini Dotto Biteko wakati
akizungumza na Waandishi wa Habari ambapo amesema lengo la Mkutano
huo ambao ni wa siku mbili ni kujadili masuala mbalimbali yanayohusu sekta
hiyo.
Akifafanua zaidi Biteko
amesema,Tanzania ni nchi mwenyeji wa Mkutano huo na kwamba itapokea
Uenyekiti wa jumuiya hiyo kutoka nchi ya Jamhuri ya Namibia ambayo inamaliza
muda wake wa kipindi cha mwaka mmoja.
Waziri Biteko amefafanua kuhusu
malengo ya Jumuiya hiyo ambapo amesema ni pamoja na kuzipatia nchi
zinazozalisha Almasi Afrika jukwaa la kuzikutanisha nchi zoteza Afrika ikiwa ni
pamoja na kubadilishana uzoefu.
Jumuiya hiyo ilianzishwa kwa mujibu
wa Azimio la Luanda, Angola na sheria za nchi za Afrika
zinazozalisha madini ya Almasi mnamo mwezi Novemba ,2006 huku
ikihusisha nchi 19 ambapo 12 kati ya hizo ni wanachama ,nchi saba ni
waangalizi.
0 Comments