📌HAMIDA RAMADHANI
IMEELEZWA Kuwa Ukatili wa Kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto wa kike Unabebwa na dhana kubwa ya Mfumo dume Umasikini na imani za kishirikiana.
Katika kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa vitendo hivyo vya ukatili Taasisi ya TGNP Mtandao imekuwa ikijihusisha na Harakati za ukombozi wa wanawake Kimapinduzi nchini Tanzanian ,Barani Afrika na kwengineko Duniani.
Taasisi hiyo ya TGNP Mtandao jana April 14 imetoa mafunzo kwa baadhi ya wabunge wanawake lengo likiwa nikuwepo kwa elimu juu ya vitendo Vya ukatili vinavyofanyika lila siku katika jamii ili nawao waende wakapaze sauti zao Bungeni hasa kipindi hiki cha vikao vya Bunge la Bajeti vinavyoendelea.
Jackline Ngoyani msongozi ni Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma ambaye ni moja Kati ya wabunge wanawake walioshiriki mafunzo ya shirika la (TGNP) Mtandao juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Amesema kupitia mafunzo hayo Wamepata uelewa mpana ambapo sasa, wanakwenda kuishauri serikali kuweka Mpango Mkakati utakaoenda mpaka katika jamii inayoishi na wanawake na watoto iliwaweze kuondokana na kutokomeza kabisa ukatili.
Naye Mbunge Viti Maalumu kupitia tiketi ya Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ester Matiko amesema kupitia mafunzo hayo Wameweza kupata elimu na kujua zaidi takwimu za Mikoa inayoongoza kwa ukatili wa kijinsia.
Sasa tumeweza kutambua serikali inatakiwa kutenga bajeti ya kutosha katika kuhakikisha mapambano dhidi ya ukatili kwa wanawake na watoto yanaendelea.
Matiko.
Kwa Upande Wake Mwasi Damas Mbunge wa Viti Maalum na ni mwakilishi wa Vijana Taifa kutoka Mkoa wa Mwanza amesema wamepewa mafunzo ya ukatili kwa wanawake na watoto lengo likiwa ni kuhakakisha wanapata uelewa juu ya vitendo Vya ukatili kitakwimu hasa kipindi hiki cha Bunge la bajeti.
" Tumeweza kubaini ni Mazingira gani ya ukatili yanatokea na na mazingira gani yamekithiri na hatua kama nchi, serikali na Asasi za kiraia zimechukua kupunguza tatizo hili,".
Na kuongeza kuwa"Mafunzo Haya yamekuja kwa kipindi Muafaka kwani wakifika bungeni tutaisemea agenda hii kwa upanda wake ili fedha itengwe kulingana na upande wa tatizo hili,"amesema Mwasi.
Aidha ametoa wito kwa
wanaharakati wakupinga ukatili na wabunge wote watumie nguvu kubwa kulisemea
jambo hilo bila kuwasahau Vijana wakike kwani ndio wameonekana wahanga wakubwa
wa tatizo hili.
0 Comments