📌BENNY MWAIPAJA, ZANZIBAR
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewahimiza vijana Visiwani Zanzibar
kuchangamkia fursa za uchumi wa blue unaotokana na shughuli za uvuvi na
uchakataji wa samaki ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhe. Masauni ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar, ametoa rai hiyo wakati akizungumza na viongozi na
baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kikwajuni akiwa
katika ziara yake ya kikazi visiwani humo.
Amesema kuwa yeye binafsi na
Mwakilishi wa Jimbo hilo katika Baraza la Wawakilishi Mhe. Nasor Ali Jazeerah
pamoja na viongozi wengine wamejipanga kutoa vifaa vitakavyotumiwa na vijana
kwa ajuili ya shughuli za uvuvi katika sekta hiyo ya uchumi wa blue ili waweze
kujitegemea kwa kujipatia kipato cha uhakika.
Tunataka tuangalie uwezekano wa kujenga mazingira mazuri ya kuwatafutia “ndoano” na siyo “samaki” na tumeandaa vitu vikubwa ambavyo sitaki niseme mapema hapa nitaondoa radha, mkawaambie vijana wa Kikwajuni kama hawatatoka kimaisha kipindi hiki hawatatoka maisha
Masauni.
Pamoja na kusisitiza masuala ya kiuchumi, Mhandisi Masauni alisema kuwa mipango mingine iliyowekwa na uongozi katika Jimbo la Kikwajuni ni kuendesha mashindano ya kusoma qoran kwa vijana na kuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki mashindano hayo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo
hilo Mhe. Nasor Ali Jazeerah, aliwaahidi wakazi wa Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar
kwamba ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita zitatekelezwa
kikamilifu.
Alitoa wito kwa wakazi wa Jimbo hilo
kushikamana, kupendana na kuacha majungu ili mipango ya maendeleo iliyopangwa
iweze kutekelezwa kwa kasi zaidi.
Aliwashukuru wananchi kwa kumwombea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ili
waendelee kuingoza nchi kwa umahili mkubwa.
0 Comments