📌FAUSTINE GIMU GALAFONI
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
ametangaza kuisha kwa siku 21 za maombolezo ya msiba wa hayati
Rais.Dk John Magufuli na kwamba shughuli za Serikali zitaanza rasmi kesho.
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na
waandishi wa Habari huku akisema Serikali itahakikisha inasimamaia
muelekeo wa utendaji kazi kama alivyoagiza Rais Samia suluhu Hassan
na kuwataka watendaji wote kutimiza majukumu yao ipasavyo.
Hata hivyo amesema wataendelea
kutekeleza malengo ya maendeleo ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM
hasa miradi mbalimbali ambayo imeanishwa katika ilani hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
ametoa shukrani za pekee kwa vyombo vya Habari nchini na kuahidi
kutoa ushirikiano.
Ikumbukwe kuwa Hayati Dk John
Magufuli alifariki dunia Machi17 Mwaka huu katika hospitali ya Mzena Jijini
Dar-es-Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ambapo alizikwa Machi26 mwaka huu
Wilayani Chato Mkoani Geita.
0 Comments