📌FRED ALFRED
SERIKALI
imewaagiza maafisa elimu kata kuhakikisha wanasimamia fedha na miradi yote
ya elimu katika shule za msingi na sekondari ili ikamilike
kwa wakati na kuleta manufaa kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa jijini hapa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa David Silinde wakati akifungua kikao cha maafisa elimu kata
nchini(UMEKTA).
“Kuhusu
usimamizi wa fedha na miradi ya elimu, kila Afisa elimu kata asimamie miradi na
fedha zote za serikali ndani ya kata yake kwa shule zote za msingi na
sekondari.
“Baadhi
yenu mnazembea kwenye usimamizi na kuisababishia Serikali hasara na
kutokuonekana kwa thamani ya fedha kwenye baadhi ya miradi inayotekelezwa
katika Kata zetu,”alisema
Silinde
alisema imebainika kuwa baadhi ya walimu
wamekuwa na mikopo mingi kupita kiasi inayopelekea kukosa utulivu kazini na
kusababisha utendaji kazi usioridhishi hivyo kila Afisa Elimu kata ahakikshe
kuwa, walimu wanaelimishwa juu ya madhara ya mikopo hiyo.
Alisisitiza
liwa maafisa elimu kata wanatakiwa kusimamia
kikamilifu ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi katika Shule za Msingi
na Sekondari kwa kuwa imebainika kuwa baadhi ya Maafisa Elimu kata hawasimamii
shule za Sekondari.
Kila Afisa Elimu Kata afanye tathmini ya maendeleo ya taaluma kwenye kata yake ili kubaini changamoto zinazokwamisha utoaji wa elimu bora ndani ya kata husika na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikisha jamii na viongozi wa kata husika
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Gerald Mweli alisema Serikali imewawezesha maafisa elimu kata
kwa kuwapa nyenzo ya usafiri pamoja na
posho ya kuwasaidia kutekeleza majukumu yao.
Alisema
hata hivyo, baadhi wamekuwa hawatimizi majukumu yeo ipasavyo ikiwemo kutokufika
kwenye shule kwa muda mrefu.
Tutakuwa na usimamizi wa karibu kuona kuwa, mnatekeleza majukumu yenu, na pale ambapo itabainika kuwa na udhaifu au uzembe, hatua kali za kisheria na kiutumishi zitachukuliwa dhidi ya wahusika,
Naibu
katibu mkuu aliongeza kuwa ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia
kwenye Shule za Msingi na Sekondari, Serikali kwa kushirikiana na Wadau
mbalimbali, Washirika wa Maendeleo na jamii imejenga vyumba vya madarasa kwenye
shule za msingi na hivyo kuongezeka kutoka 115,665 mwaka 2015 hadi kufikia
136,292 mwaka 2020.
“Wakati
huo huo, idadi ya shule za msingi imeongezeka kutoka 16,899 mwaka 2015 hadi
17,804 mwaka 2020 na shule za Sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi 5,330
mwaka 2020,”alisema.
0 Comments