📌AMIDA RAMADHANI
WAKULIMA wa zao la Mtama Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma sasa wana uhakika wa Soko lao baada ya kuingia Kilimo cha mkataba na kampuni ya kuzalisha bia nchini Tanzania Breweries Limited (TBL).
Aidha,TBL itatoa huduma kwa Mkulima ikiwemo Mbegu bora lakini pia Soko la uhakika ambapo Mkulima hatapita kwa walanguzi kama iliyokuwa,kabla.
Akiongea kwenye ziara ya kukagua zao la Mtama la Kilimo cha Mkakati katika kijiji cha Nghumbi Wilayani Kongwa Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda amesema kupitia TBL wakulima watapewa fursa ya kulima na kuwa na uhakika wa masoko kutoka bei ya mauzo ya Sh300 kwa kilo moja hadi Sh550 kiwango hicho.
Mtama sio zao la chakula bali ni la biashara na hatua hii ni mojawapo ya kuwahamasisha wakulima wengine kuendelea kulima zao la Mtama
Profesa Mkenda.
Aidha amebainisha kuwa licha ya wakulima wa Mtama kukumbwa na changamoto ya mvua ya kutosha,masoko,Mbegu bora lakini pia Serikali ipo Kwenye mchakato wa kutatua changamoto hizo.
Hata hivyo,ametoa wito kwa wakulima watakaopewa Mbegu na huduma waheshimu mkataba huo kwani kumekuwa na baadhi yao ukifika Mwisho waheshimu masharti ili wote wafikie Malengo
Naye Yusuph Malenda mkulima wa zao la Mtama katika kijiji cha Nghumbi Wilayani Kongwa amesema kwamba wamepatiwa Mbegu za Msingi katika mradi wa kuendeleza zao la Mtama na ubalozi wa Ireland hapa Nchini Tanzania na kutekelezwa na shirika la Mpango wa chakula duniani WFP kupitia Serikali ya halmashauri ya wilaya hiyo .
Malenda amesema shamba lake lina ukubwa wa hekari 2 ambapo anategemea kuvuna kilogram 200 za Mtama ambapo ataweza kuwauzia wakulima wenzake 100 kwa shilingi 3000.
Zao la Mtama ndio zao mtambuka kwa kijiji cha Nghumbi kwani mimi ni mmoja wa wakulima wa mfano niliye lima kwa Mbegu bora na manufaa yake ndio kama haya yanayoonekana
Mkulima Malenda.
Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilayani hapo Pascalina Duwe amesema kuwa Wilaya ya Kongwa imedhamilia kuondoa tatizo la upungufu wa chakula na kuhakikisha Usalama wa chakula na kipato unafikiwa katika ngazi ya kaya.
Aidha amesema katika kufanikiwa adhima hiyo Wilaya imeendelea kufikia mkazo zaidi katika utekelezaji wa Kilimo cha mtama kinachohimili zaidi athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.
"Wilaya ya Kongwa ni Kati ya wilaya inayotekeleza mradi wa Kilimo himilivu wa Mtama kuanzia msimu wa kilimo2018/2019 na utahitimishwa 2021 mnamo mwezi June,
Mradi huo unatekelezwa na Halmashauri ya wilaya ya Kongwa kwa shirikiano wa shirika la WFP akiwa mfadhili Mkuu wakati mtekelezaji akiwa ni shirika la Farm Africa
Pascalina Duwe
Vilevile,Malengo makuu
ya mradi huo ni kuwainua wakulima wadogo na kuongeza uzalishaji (tija),uhakika
wa chakula kwa Mkulima(zero hunger)upatikanaji wa masoko ya uhakika na
kuhakikisha Mkulima anatuamia dhana bora za utunzaji na uhifadhi.
0 Comments