KATAMBI 'AWASHUKIA' MAAFISA KAZI

 


📌DEVOTHA SONGORWA

 NAIBU Waziri,Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia  Kazi,Vijana na Ajira  Patrobasi Katambi  amewataka maafisa kazi kusimamia vyema taratibu na sheria kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao badala ya kuwa sehemu ya migogoro maeneo ya kazi.

Naibu Waziri Katambi amesema hayo jana alipokutana na maafisa kazi katika kikao kazi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye ulemavu,Jenista Mhagama alipomtaka kukutana na maafisa kazi.

Alisema kwamba uwajibikaji wa kuridhisha wa maafisa kazi katika maeneo yao waliyopangiwa utarahisisha utatuaji wa changamoto za wafanyakazi na kupunguza malalamiko ya wafanyakazi pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa waaajiri kutambua wajibu wao kwa wafanyakazi wao.

“Kesi zikiwa nyingi ina maana kuna ucheleweshaji wa mashauri n pia ni taarifa kwamba afisa kazi wa eneo hilo hafanyi kazi vizuri kwa sababu kesi utakuta ni 'unfair termination' lakini kama unawapitia watu wako vyama vya wafanyakazi viko imara, afisa kazi yuko imara manake hawa waajiri watakuwa na hiyo elimu na watakjua kwamba wakifukuza mfanyakazi bila kufuata utaratibu sheria zitachukulia,”alisema Naibu Waziri Katambi.

 Pia Naibu Waziri huyo aliagiza kutekelezwa kwa agizo la uendeshaji wa “Labour Clinic” ya kila ijumaa ya mwisho ya kila mwezi ambayo lengo lake ni kuhakikisha migogoro inatatuliwa haraka pamoja na kusimimiwa kwa maslahi yao.

“Kila ijumaa ya mwisho wa mwezi kutakuwa na labour clinic kwenye labour clinic hizi tunazitekeleza?na jamii imeshajua kwamba zinafanyika kwa sababu ndiyo maelekezo ya wizara wafanyakazi wakasimamiwe na kuangaliwa kwenye maslahi yao sasa tukiwa na hivyo vikao itawasaidia wafanyakazi wengi wanaolalamika katika mitandao kujua pa kwenda wakati,”alieleza Naibu Waziri huyo.

Akizungumzia vibali vya kazi kwa njia ya mtandao alibainisha kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu inatarajia kuzindua mfumo wa mtandao wa kuomba vibali vya kazi kielektroniki  hivi karibuni hatua itakayosaidia kupungua urasimu  wakati wa kuomba vibali hivyo.

“Ofisi ya Waziri Mkuu itapeleka mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya vibali vya kazi ambayo yatapelekwa bungeni kufanyiwa marekebisho ili ilete unafuu na uharaka pamoja na hilo mfumo wa kielektroniki sheria inataka kibali kitoke ndani ya siku 14 na kisivuke siku 14 na kama ni rufaa ziwe ndani ya siku 30,”alieleza.


Akigusia baadhi ya mapungufu yanayojitokeza  nje katika utekelezwaji wa sheria ya vibali alisema wapo baadhi ya waajiri amabo ndiyo wanapaswa kuwaombea vibali wafanyakazi wao wamekuwa na tabia ya kutumia mawakala au madalali kufuatilia vibali vya kazi jambo ambalo limekuwa na sura tofauti kutokana n akutozwa fedha hali inayosababisha udanganyifu mkubwa.

“Ukienda kule mwajiri unaanza kupangwa hapa kuna hili unajua huna sifa kwa hiyo inabidi tuliweke vizuri kisheria lakini tuangalie hela hapa ya kumpa afisa kazi au Katibu wa Waziri halafu mwisho wa siku anakuja ofisini anafuata taratibu zilezile kule mwajiri anaamini kwamba ili upate lazima kuwe na fedha matokeo yake inaoneka huku kuna rushwa sasa nitoe onyo tutachukua hatua kama Wizara,”Alifafanua.

Kuhusu mapungufu ya ndani ya watendaji alisema wapo baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazoea kutokana na kukaa muda mrefu katika kituo chake cha kazi hali inayosababisha kutengeneza mtando mkubwa na watu wengine hatimaye mtu kukosa haki yake na maamuzi kucheleweshwa kumfikia mhusika.

“Tutawabaidilisha hata kila wiki mtahama vitu au mtafanya kwa kuswap  kwa sababu kumbe ukikaa kwa muda mrefu unatengeneza network tutawapangua pangua kweli kweli nina mafano wa vibali vingi watu wanalalamika mtu anakuja kuomba kibali anambiwa njoo kesho kumbe kimeshaenda kwa kamishina ameshatoa maamuzi hayatolewi kuja kuyapata either amepewa au hajapewa inachukua wiki mbili faili limewekwa chini ya meza,”alieleza.

Hata hivyo alizungumzia suala la fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo aliwasisitiza kuongeza jitihada ya uandiksihaji wa wanachama katika mifuko yao hatua itakayosaidia kuongeza mapato ya ndani.

Post a Comment

0 Comments