📌MWANDISHI WETU
MKUU
wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt Bilinith Mahenge amewataka Wakazi wa Mkoa wa Dodoma
kuchangamkia elimu inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
kwa kuwa ina umuhimu mkubwa katika kujikwamua kiuchumi.
Dkt.
Mahenge ameyasema hayo leo Aprili 17, 2021 wakati akifungua mafunzo ya siku
mbili kwa Wakazi wa Dodoma katika Ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Zimamoto,
Jijini Dodoma.
Akizungumza
katika ufunguzi huo Dkt. Mahenge amewaeleza washiriki kwamba, ili kuweza
kufanikiwa katika biashara ni vyema biashara au kazi husika kuwa imerasimishwa
na kutambulika kisheria.
Hatua ya kwanza ya kufanikiwa katika biashara ni kuirasimisha biashara na ikwa inatambulika kwa mujibu wa sheria. BRELA wapo hapa Dodoma kwa siku mbili kwa hiyo hii ni fursa kubwa na adhimu
Dkt. Mahenge.
Naye
Msimamizi wa Kanda ya kati na Ofisi ya BRELA mkoani Dodoma, Bw. Gabriel
Girangay amesema kwamba licha ya elimu hii kwa wote inayotolewa kwa siku mbili
lakini pia ofisi zipo tayari kwa ajili ya kuwa hudumia.
Ofisi ya BRELA mkoani Dodoma ipo tayari kuwahudumia na inafanya maandalizi ya kufika katika Wilaya zote tisa za Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi katika maeno yao kuhusu huduma zetu
Girangay
BRELA imeandaa mafunzo ya siku mbili (tarehe 17 na 18/04) ili kuwapa wajasiliamali elimu ya kurasimisha biashara zao ili kuweza kupata fursa za kibiashara.
UMEISOMA HII?👇👇👇
0 Comments