SERIKALI imesema
inatarajia kukamilisha ujenzi wa daraja la Kiyegeya, mkoani Morogoro, hivi
karibuni, ambalo lilibomoka mwezi Machi, mwaka
2020 kutokana na mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha.
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo
katika mkoa huo, Waziri huyo amesema kuwa ujenzi huo unatekelezwa na Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS), kwa kushirikiana na Wakandarasi wengine kwa
mtindo wa ‘Force Account’.
Ningependa kuwapongeza TANROADS kwa kazi nzuri walioifanya tena kwa ufanisi mkubwa, hivyo, tunatarajia baada ya miezi michache daraja hili litakamilika ili wananchi waweze kulitumia tena, mapema iwezekanavyo
Chamuriho.
Aidha, Chamuriho amesema kuwa ametembelea sehemu wanayotengeneza mihimili mikuu ya daraja hilo na kufafanua kuwa katika miezi michache ijayo kazi ya kuinyanyua na kuiweka juu mihimili hiyo itafanyika, na baada ya hapo utafuata ujenzi wa barabara za maungio mbili ambapo moja itakuwa na mita 1000 na nyingine mita 800, upande wa Dodoma na upande wa Morogoro.
Ameongeza kuwa ujenzi
wa daraja hilo lililopo katika barabara ya Morogoro - Dodoma ni muhimu, kwani
ndio njia pekee inayounganisha mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro na mikoa ya Kaskazini ya kati na hata kuelekea
nchi za jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.
Ametoa rai kwa Mameneja
wa TANROADS katika mikoa yote nchini kuhakikisha wanaendelea kukagua madaraja yote ikiwemo
kingo zake, pamoja na kukagua mito yote inayoelekea kwenye madaraja hayo na kuisafisha ili kudhibiti matatizo ya kukatika
kwa madaraja.
Kwa upande wake, Meneja
wa TANROADS, mkoa wa Morogoro, Mhandisi, Kolante Ntije, amesema kuwa ujenzi
unaendelea vizuri na mpaka sasa umefika asilimia 58.
Kama alivyosema Mheshimiwa Waziri, wakati wowote tunatarajia kuweka mihimili hapa juu, na niwahahakishie watumiajia wa barabara hii kuwa hatutachukua muda mrefu kuikamilisha kazi hii
Mhandisi Ntije.
Daraja hilo ambalo lilibomoka mwezi Machi, mwaka jana na kuleta msukosuko mkubwa na hivyo kupelekekea Serikali kujenga daraja la muda pembeni yake, linajengwa upya na Serikali, ambapo ujenzi wake unagharimu shilingi Bilioni 6.9.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
0 Comments