📌SALEH RAMADHANI.
CHIFU wa kabila la Wagogo, Henry Mtemi Mazengo wa pili ameiomba serikali hususani wakuu wa wilaya kutembelea vijijini ili kutatua matatizo yanayo wakabiri wananchi Wao.
Hayo yamebainishwa leo wakati akitatua mgogoro wa mpaka kati ya vijiji vya Chitemo, Ngalamilo pamoja na ibeleje ambapo. Alisema kumekuwa na kundi la viongozi kutoka halmashauri wamekuwa wakiwakingia vifua viongozi wa vijijini na kusababisha viongozi hao kuwa chanzo cha kuchochea uvunjifu wa amani na kusababisha uchochezi wa migogoro ya kugombania ardhi kati ya kijiji na kijiji.
Chifu Mazengo alivitaja vijiji vya Chitemo, Ngalamilo na Beleje ambavyo viko kata ya Mima Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, ni moja ya wahanga wa tatizo hilo lililodumu kwa takribani miaka 5 lililo dhoofisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.
"Ningependa kusisitiza hasa viongozi ni kwanini wamekuwa chanzo cha ugombanishi kwa wananchi huyu kiongozi wa Beleje hana maan ya kuwaongoza nyinyi kama anakua chanzo cha kuwagombanisha" amesema Chifu
misitu inateketea na wanao iteketeza ni wanakijiji wenyewe hii ina maana gani kuishi vijiji tofauti ni lazima muwe na alama zitakazo watofautisha kimpaka na sio katika shughuli zenu
Mazengo alisema chanzo kikuu cha mgogoro katika vijiji hivyo kinatokana na kiongozi kutoka kijiji cha beleje alie washinikiwa wananchi wake kufanya uharibifu wa maeneo ambayo wanatumia majirani zao.
Alisisitiza kuwa tangu miaka ya nyuma viongozi wa vijiji hivyo walikua wakitawala maeneo hayo kwa amani na utulivu lakin kuja kwa mwenyekiti huyo wa kijiji amekua akifanya uchochezi huo kwa maslahi yake binafsi huku akijitamba kulindwa na viongozi kutoka Wilayani.
"Ni jambo la aibu sana kwa jamii mnafanya mambo ya hatari vizazi vyenu vitakuja kurithi nini kama leo hii mnaharibu mazingira kwa shinikizo la mtu ambaye mlimchagua wenyewe na mnaweza mkamtoa hata nafasi aliyo nayo hakika sita lifumbia macho swala hili". amsema Mazengo.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Chitemo, Yohan Mkwai, alisema walikua wakifuatilia suluhisho la mgogoro huo kutoka Wilayani pasipo kupata ushirikiano wa kiongozi yoyote ijapo kuwa mkuu wa Wilaya aliwatuma maafisa ardhi kuja kupima eneo hilo.
Amesema wanakijiji hawana mgogoro wowote kuhusu maeneo hayo bali chanzo cha uchonganishi kinatoka katika uongozi wa Kijiji cha Beleje ambapo mwenyekiti hutuma vijana kwenda kuharibu maeneo ya vijiji vya Chitemo na Ngalamilo kwa kukata miti na kuharibu mazao yao.
"Kwa kweli tumechoshwa sana na suala hilo tumejitahidi kulifuatilia kiundani lakini kila tukifika ngazi ya Wilaya huwa tunazungushwa sana hakuna hatua yoyote inayo chukuliwa zaidi ya kusema tutakuja kutembelea kuona hali ilivyo". Alisema Mwenyekiti.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Ibeleje Mh Baraka Habari amebainisha kuwa mgogoro huo umeleta madhara makubwa sana hususani uharibifu wa miundombinu jambo ambalo limesababisha mashamba mengi kuharibika,hivyo alisema hatua kali zimeanza kuchukuliwa kwa wale watakao bainika wanaharibu misitu watawanibishwa.
Wizara ya Ardhi inapaswa kufuatilia kiundani
mambo ya migogoro ya ardhi hususani vijijini kumekuwa na kero nyingi ambazo
ukifuatilia chanzo chake kinasababishwa na baadhi ya viongozi wa juu kwa
maslahi yao binafsi.
0 Comments