JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA KILIMO
Anuani yaSimu: “Kilimo Dodoma” Idara ya Utawala,
Nambari: +255 26 2321407 Mji wa
Serikali Mtumba,
Fax: +255 26 2320037 S.L.P. 2182,
Email:
ps@kilimo.go.tz DODOMA.
TAARIFA
KWA UMMA: WAZIRI MKENDA AZINDUA MFUMO WA KIZIMBA KUVUTIA VIJANA KATIKA KILIMO
Morogoro 16.03.2021
Waziri wa Kilimo Prof.
Adolf Mkenda amezitaka taasisi za fedha nchini kutoa mikopo yenye masharti
nafuu ili kuwavutia vijana wengi kujikita katika kilimobiashara kupitia mfumo
wa Kizimba ‘Business Model’ unaoratibiwa na Taasisi ya SUGECO.
Akizundua mfumo huo mjini Morogoro leo (16.03.2021) Prof. Mkenda mbali
ya kuupongeza,amesema mfumo wa Kizimba
utawezesha vijana wengi kujiunga pamoja kama ushirika na kutumia ardhi
kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kilimo kwa usimamizi wa wataalam
wa taasisi hiyo.
“Wito wa serikali kwa
taasisi za kifedha hapa nchini nikutoa mikopo yenye riba nafuu ili waweze
kuanzisha shughuli za kilimo kupitia mfumo huu wa kizimba ambapo utasaidia kuongeza tija na uzalishaji mazao ya kilimo
hali itakayochochea ukuaji wa ajira na kuongeza kipato kwa vijana ” alisema
Waziri Mkenda.
Ili kukuza tija na
uzalishaji kwenye sekta ya kilimo Prof. Mkenda amesema wizara yake itaendelea
kuhamasisha kujengwa kwa miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuhakikisha
upatikanaji wa pembejeo bora na huduma za ugani hatua itakayokuza tija kwenye
kilimo.
Aliongeza kusema kuwa
taasisi ya SUGECO inayoundwa na wahitimu inafanya kazi nzuri ya kuwaunganisha
vijana wanaofanya kazi za kilimo kwa kuwapatia mafunzo kwa vitendo na
kuwaunganisha na masoko.
“Sekta ya kilimo
kinachangia chini ya theluthi moja kwenye pato la taifa (28%) na kwa upande wa kilimo mazao bado mchango wake ni chini na takribani
theluthi mbili ya nguvu kazi ya watanzania inajishughulisha na kilimo hivyo
tafsiri yake ni kuwa tija yetu bado ipo chini..Tunataka tuongeze tija ili
kilimo kichangie zaidi kwenye ukuaji wa uchumi” alisisitiza Prof.Mkenda
Kwa upande wake Makamu Mkuu
wa chuo Kikuu cha Sokoine Prof.Raphael Chibunda alisema chuo hicho kitaendelea
kushirikiana na wizara ya kilimo kusukuma na kubadilisha mfumo wa kilimo kuwa
wa kibiashara ambapo sasa kiefanikiwa kuanzisha mashamba biashara kwenye maeneo
yote ya chuo.
Prof. Chibunda aliongeza
kusema taasisi ya SUGECO inafanya kazi zake kwa kutoa mafunzo ya vitendo
kupitia vitalu nyumba zaidi ya 100 kufundisha vijana stadi za kilimo biashara
hatua inayochangia kukuza ajira na kipato kwa vijana.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
SUGECO Revocatus Kimario alisema mfumo wa kizimba Bussines Model ulizindiliwa
utawezesha vijana wengi kukutana na wadau wa kilimo ikiwemo taasisi za fedha
kwa ajili ya mitaji na wataalam wa ugani hatua itakayokuza uzalishaji wa mazao
.
Kimario alisema Kizimba
Bussiness Model unalenga kubadili fikra na mitizamo ya vijana kuhusu
kilimo ambapo itafanya waone kilimo ni
ajira kama zilizvyo ajira zingine kupitia vikundi kwenye halmashauri ambapo
kilimo vizimba itaanzishwa.
“Mfumo wa kizimba
utapunguza vihatarishi kwa wakulima kwani watapata huduma kwenye eneo moja
chini ya uratibu wa wataalam na uwepo wa uhakika wa soko ambapo tatizo la ajira
litapungua kwa kiasi kikubwa” alisema Kimario.
Mwisho
Imetolewa na;
Wizara
ya Kilimo
MOROGORO
0 Comments