📌MWANDISHI WETU
KATIKA uhai wake kama kuna kitu Hayati Dkt. John
Pombe Magufuli alikipigania na kukipangia kukipigania zaidi kikue zaidi ni
sekta ya sanaa.
Katika kampeni zake mwaka jana tu neno wasanii
lilikuwa kinywani mwake sana, mwaka 2015 bila kusahau pia na ndiye Rais wa
kwanza kuunda wizara yenye sekta ya sanaa kama sekta inayojitegemea.
Leo hatuko naye mtu huyu Dkt. John Pombe Magufuli, bingwa katika kuipigania sekta ya sanaa, anapaswa kuimbiwa, nyimbo za maombolezo, nyimbo za kumwombea pumziko la amani na la milele.
"Hivyo Machi 25 (leo) kuanzia saa 10 kamili
jioni hadi saa moja katika uwanja wa Magufuli hapa Chato tumewapa nafasi
wasanii wote watakaoweza kufika Chato na waliokwishafika Chato kumuimbia
Magufuli kwa nyimbo mbalimbali za maombolezo walizozitunga mmoja mmoja na kama
makundi," alisema Dkt. Hasaan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa akiteta jambo na mmoja wa Wasanii waliofika kumuaga Hayati Dk.Magufuli. |
Tayari wasanii zaidi ya 25 wako wilayani Chato
kushiriki shughuli mbalimbali za kumuaga Magufuli.
"Serikali imeridhia ratiba hii ya wasanii
kwanza kupata nafasi ya kumuaga kiongozi wao lakini pili baadaye kumwimbia
katika tukio maalum litakalokuwa mbashara katika redio na TV mbalimbali nchini.
Hii ni heshima kubwa kwa wasanii na ni heshima kubwa kwa Mzee wetu Dr.
Magufuli," alisema Dkt. Abbasi.
0 Comments