📌MWANDISHI WETU
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza Meja Jenerali Suleimani Mzee amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Francis Lutalala, ambaye ni Mratibu wa Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF) Jijini Dodoma kwa lengo la kuona uwezekano wa kuboresha afya ya Watumishi wa Jeshi hilo pamoja na Wafungwa na Mahabusu waliopo Magerezani.
Jenerali Mzee amesema kuwa amefurahishwa na ujio wa Dkt. Lutalala, kwakuwa umetoa mwangaza kuelekea mpango wa kupunguza gharama za matibabu kwa Wafungwa kutokana na bima hiyo kuchukua watu Sita kwa gharama nafuu ya Shilingi Elfu 30 kwa mwaka, huku akiweka wazi nia yake ya kujenga Hospitali kubwa katika eneo la Msalato yalipo Makao Makuu ya Jeshi Hilo.
Niseme tu nimefurahishwa na ujio wako, hii bima nimekubaliana nayo na Nina mpango wakujenga hospitali kubwa kwahiyo ninaimani Mambo yataenda vizuri na tutaboresha zaidi Afya za watu wetu
Kamishna Meja Jenerali Mzee
Kwaupande wake Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Gereza Msalato Dkt. Mpamba Juma amesema, wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa wananchi wa maeneo ya jirani pamoja na Wafungwa kwa kushirikiana na CHF.
Sisi tumejipanga vizuri Sana katika kutoa huduma, hivyo kuja kwa CHF kutapelekea huduma kuwa Bora zaidi kwakuwa wanachi wengi Sasa wenye bima hii wataanza kuja katika Zahanati yetu
Dkt. Mpamba Juma
Akizungumzia mafanikio ya ujio wake
Dkt. Lutalala mratibu wa CHF amesema, anashukuru kukutana na Jenerali Mzee na
kufanya nae mazungumzo chanya, ambapo amemueleza namna walivyo itangaza
Zahanati ya Gereza Msalato na Mafanikio yanayoanza kuonekana kwa muda mfupi,
huku akiahidi kulichukua wazo la kujenga Hospitali kubwa zaidi na kulifikisha
kwa Mkuu wa Mkoa ili kupata msaada zaidi.
0 Comments