📌FAUSTINE GALAFONI.
Vyama vya Ushirika
hapa nchini vimetakiwa kuanzisha mifuko ya utafiti hali itakayosaidia kutatua
changamoto za wakulima kwa ufasaha.
Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Naibu katibu mkuu wizara ya kilimo Prof.Siza
Tumbo wakati wa ufunguzi wa kongamano la kwanza la tafiti za ushirika ambalo
limeandaliwa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini[TCDC].
Prof.Tumbo amesema
fedha za kutegemea wadau kutoka nje zimekuwa na masharti magumu hivyo ili
kuondokana na vikwazo ni vyema kuanzisha mifuko ya utafiti.
“Tume ya Ushirika na
vyama vikuu vya ushirika mkianzisha mifuko ya fedha za utafiti itasaidia sana
,maana fedha hizi za kutegemea wadau wan je ya nchi wanakuwa na masharti mara
niandikie andiko kwa kiingereza ,muwasilishe kwa lugha ya kiingereza ,amesema.
Aidha,Prof.Tumbo
amesema licha ya kuwezesha tafiti nyingi nchini,bado tafiti hizo
hazina majibu ya kero za wananchi hivyo kuwataka watafiti kutumia muda
mwingi kufanya tafiti za masuala ya masoko huku pia akionya kwa baadhi ya wana
Ushirika wanaoingia kwenye vyama hivyo kwa lengo la kujitajirisha .
Naye Mrajisi wa vyama vya ushirika nchini
Dkt.Benson Ndiege amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni fursa kwa kuwa
limewakutanisha wadau wa maendeleo ya ushirika kukutana na wanachama
,viongozi watendaji hivyo kuwa na matumaini zaidi katika kuleta matokeo ya
tafiti mbalimbali za ushirika zilizowahi kufanyika na mapendekezo yake na kupata
utatuzi wa changamoto zinazoikabili sekta hiyo.
Sambamba na lengo kuu,Mrajis huyo ameainisha matarajio mengine kwenye kongamano hilo ni kupata mambo yatakayoibuliwa na washiriki ikiwa ni pamoja na vipaumbele vitakavyoainishwa vitafanyiwa utafiti ambapo maamuzi yake yatakuwa shirikishi ili kurahisisha utekelezaji.
Kwa upande wake Meneja mkuu
chama cha ushirika cha mradi wa pamoja zao la tumbaku[TCJE]Bakari Hussein
amesema bado suala la elimu lipo chini kwa wana ushirika hivyo inahitajika
zaidi na si kwa viongozi pekee
ANGALIA PIA KWENYE CPC TV
👇👇👇
0 Comments