📌PENDO MANGALA.
TAASISI ya utafiti juu ya kupunguza umaskini nchini (REPOA)imezindua vitabu viwili,vinavyohusu "Mpito wa Vijana kutoka Shule kwenda kazini Tanzania," na jingine ni "Kuwawezesha Wanawake Nchini Tanzania katika muktadha wa Mageuzi ya Sera ya Jamii ya Kisasa".
Akizungumza katika uzinduzi wa vitabu hivyo, uliofanyika Jijini Dodoma,Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk Donald Mmari, amesema katika miaka ya hivi karibuni, walifanya tafiti na mafunzo ya ufundi kwa vijana, ikiwemo uwezeshaji wa wanawake ambao vitabu hivyo vinategemeana.
Amesema, wakati wa utekelezaji wa utafiti huo, Repoa ilifanya kazi na wadau tofauti pamoja na Taasisi za Serikali kwenye maeneo hayo ili kupata tafiti zenye tija.
Dk.Mmari amefafanua kuwa matokeo ya utafiti huo yalisambazwa kupitia warsha na mapendekezo yaliyotolewa kwa Taasisi zinazohusika kuwezesha uundaji wa Sera za ushahidi na kuarifu mikakati anuwai ya maendeleo.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za umma, Naghenjwa Kaboyoka ambaye alimwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema suala la utafiti kwa sasa ni changamoto kubwa jambo linalopaswa kutiliwa mkazo zaidi .
Kaboyoka amesema suala la utafiti bado ni shida kubwa, sio kwa madaktari tu au walimu,Bali no kote na kwamba eneo hilo linahitaji suluhisho la kudumu," amesema.
"Lazima tujitafakari katika Karne hii ya Sayansi na Teknolojia tuliyonayo Sisi Watanzania kuhusu suala zima la kufanya utafiti halikwepeki ni wakati muafaka Sasa wakuleta tija kupitia tafiti,"alisema.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa Taasisi na wadau wengine kuzingatia eneo hilo ili kuweza kuleta maendeleo kwa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Mwishoo.
0 Comments