📌RHODA SIMBA
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais
Menejimenti ya utumishi na utawala bora Deogratius Ndejembi
ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini
(TAKUKURU)kuongeza nguvu kwenye kesi za ubakaji na mimba za utotoni
ambazo zimekuwa zikiminywa kwenye ngazi za chini na kusababishwa wahanga
kukosa haki zao.
Ameyasema hayo leo jijini hapa
wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa viongozi wa Taasisi
hiyo.
Amesema hivi karibuni serikali
imegundua kuwa kumekuwa na mtindo ambao sio mzuri kesi nyingi zinazohusu
rushwa ya ngono , ubakjaji, na mimba za utotoni zimekuwa zikiharibika na
kupoteza ushahidi.
“Serikali imejipanga kuhakikisha kesi
zote zinazohusu rushwa ya ngono aendelezwa na kama kuna mzazi
atabainika na kosa la kumaliza kesi hizo atachukuliwa hatua
kwasababu sheria ipo inayomtaka kila mzazi kutimiza wajibu wake,
“Nasisitiza kama kuna mzazi anafanya
hivyo atambue kuwa anafanya kosa kisheria na wanakuwa wanalea kosa la rushwa ya
ngono na ubakaji kuendelea kushamili katika jamii,”alisema
Ndejembi amewaagiza TAKUKURU katika
mipango mikakati yao ya mapambano ya rushwa kuelekeza kwenye vyuo
vyote nchini kuhakikisha wanamaliza suala la rushwa ya ngono ambako kwa kiasi
kikubwa imeshamili.
Mmefanya vizuri kwenye utafiti mliofanya ndani ya vyuo vikuu viwili yaani UDOM na UDISM sasa ni wakati mwafaka nguvu zenu mkazielekeza kwenye vyuo vyote nchini kwani bado tatizo la rushwa ya ngono lipo hata huko
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
TAKUKURU Brigedia Jenelali John Mbungo ametaja mipango mikakati ya miaka mitano
ijayo kuwa ni kuhakikisha wanatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM) ikiwa
ni pamoja na kuboresha mfumo wa utendaji kazi.
Mkurugenzi wa TAKUKURU Brigedia Jenelali John Mbungo akitoa neno |
Amesema katika awamu hii ya pili sasa
ni wakati wa kutekeleza maagizo yanayotolewa na Rais Dk John Magufuli na
kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake bila kuonewa.
“Tumejipanga katika awamu hii ya pili
tutahakikisha tunamaliza tatizo la rushwa ya ngono ambalo kipindi cha nyuma
ilikuwa imeshamili hasa katika taasisi za elimu na makazini, na kuhakikisha
wananchi wanapata elimu kuhusu kutoa na kupokea rushwa,”alisema
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk
Bilinith Mahenge ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kusimamia na kuziba
mianya ya rushwa kwenye nyanja zote.
Ilikujenga nchi iliyoendelea lazima upambane na rushwa mabae ndio adui mkubwa wa maendeleo katika nchini nashuru serikali imejitaidi na inaendelea kujipanga kudhibiti
Kikao hicho kilichokutanisha
watendaji wa TAKUKURU nchi nzima kina lengo la kutatua changamoto
zinazowakabili watendaji wa taasisi hiyo sambamba na kuweka mikakati ya mapambano
ya rushwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
0 Comments