📌DEVOTHA SONGORWA.
WIZARA ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeendelea na mchakato wa kujadili mapendekezo ya kutungwa kwa sheria ya Tehama.
Akizungumza wakati wa kikao cha kujadili
mapendekezo ya kuundwa kwa sheria ya Tehama, dokta Zainab Chaula amabaye ni Katibu mkuu wizara ya
Mawasiliano na Teknolojia ya habari amesema kuundwa kwa sheria ya Tehama
kutasaidia mambo mengi katika nyanja mbalimbali kiuchumi,kiusalama na maendeleo
ya teknolojia.
Amesema Wizara imejipanga kufanya mambo
makubwa kupitia uundwaji wa sheria ya Tehama ndiyo maana ya kuandaa kikao
maalum leo na wadau ili kupata maoni mbalimbali ya uboreshaji wa miundombinu ya
mawasiliano.
“Kuundwa kwa Wizara mpya ya Mawasiliano na
Teknolojia ya habari lengo ni kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wake
ikiwemo kuboresha vyombo vya mawasiliano vilivyo chini ya wizara kwa kuimarisha
mifumo ya Tehama ’’ alisema Chaula.
Pia katibu alisema Tanzania ishafikia uchumi
wa kati sasa kwa hiyo kupitia sheria ya Tehama ni mchakato wa kufika uchumi wa
juu na pia ikumbukwe sheria hii ni ya muda mrefu kinachofanyika ni kuiboresha
kwa michango kutoka kwa wadau.
Kwa upande wake Lugano Rweitaka Mkurugenzi wa
kitengo cha sheria katika wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari alisema
kwa sasa mambo mengi yanafanyika kwa msaada wa teknolojia ikiwemo
biashara,mikutano na elimu hivyo basi Wizara kupitia vyombo vyake kama shirika
la posta na kampuni ya mawasiliano ya simu (TCCL) vitakuwa mihili mhimu.
Hata hivyo kupitia mkongo wa taifa ni moja ya
michakato ya uimarishaji wa teknolojia ya mawasiliano ili kusaidia kupanua wigo
wa sekta hii ikiwa ni njia ya kupambana na mambo mbalimbali mtandaoni ikiwemo
makosa ya kimtandao.
“Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ni
moja ya vyombo vilivyoboreshwa katika mfumo wa Tehama na utendaji wake ni
ishara ya maendeleo ya teknolojia nchini kwa hiyo sheria ya Tehama na itakuwa
na mchango mkubwa” amesema Rweitaka.
Mhadhili wa Chuo cha teknolojia ya habari
Nkundwe Moses ni alisema uwepo wa wadau kutoka wizara mbalimbali serikalini na
wataalamu kutoka vyuo vikuu ni ishara ya utekelezaji wa kujadili mapendekezo ya
kutungwa kwa sheria ya Tehama itakayo kuwa na mashiko kwenye jamii.
“Lakini Tehama ni moja ya vitu mhimu sana
duniani kwani licha ya kuwepo kwa ulinzi ,kuboreshwa kwa mifumo ya mawasiliano
kutasaidia kuimarisha ulinzi mtandaoni kwani matumizi kuna mengine yapo kinyume
na utaratibu” amesema Moses.
0 Comments